Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 TAARIFA ZA YANGA kuhusu kujitoa kushiriki michuano ya kagame bado haijathibishwa ambapo katibu wa timu hiyo beno njovu amesema hadi sasa bado wanasubiri taarifa toka CECAFA kuhusu kushiriki michuano hiyo,licha ya hawali kocha wa timu hiyo maximo kusema kuwa kikosi chake bado hakipo tayari kushiriki mashindano kwa kuwa nusu ya wachezaji wa timu hiyo wapo tukuyu na timu ya taifa ya Tanzania.

Yanga SC ambayo kwa sasa inayofundishwa Marcio Maximo anayesaidiwa Leonardo Neiva, wote Wabrazil na mzalendo Salvatoty Edward, imetwaa mara tano taji la michuano hiyo, 1975 visiwani Zanzibar, 1993 na 1999 mjini Kampala, Uganda na mara mbili mfululizo pia 2011 na 2012 mjini Dar es Salaam.

Michuano ya Kigali mwaka huu, ilikuwa ni fursa kwao kujaribu kusawazisha rekodi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC waliotwaa mara sita, 1974, 1991 mjini Dar es Salaam, 1992 visiwani Zanzibar, 1995, 1996 mjiji Dar es Salaam na 2002 Zanzibar tena.


Chapisha Maoni