Chuo kikuu
kishiriki cha mkwawa mkoani Iringa kinatarajia kuandaa mashindano ya michezo
mbali mbali ya kumwezi mtwa mkwawa yatakayofanyika tarehe 24 mwenzi wa kumi na
moja mwaka huu.
Michezo ambayo
itakuwepo katika mashindano hayo ni pamoja na mpira wa miguu,riadha,mpira wa
pete,kikapu na michezo mengine mengi baada ya kupata udhamini katika mashindano
hayo.
Akizungumza na
Jelamba viwanjani hii leo waziri wa michezo serikali ya wanafunzi mkwawa maguluko dogulas alisema kuwa wanakaribisha
makampuni mbali mbali mbali kudhamini mashindano hayo ili kuweza kufanikisha
mashindano hayo kwa asilimia zote kwa kuwa bila udhamini watashindwa kufikia
malengo ya mashindano hayo.
Kwa upande
wake Anna Thalia mwalimu wa chuo kikuu cha mkwawa aliongeza kuwa chuo cha
mkwawa toka kianzishwe wamesoma wanafuzi wengi sana ambapo kuanzishwa kwa
mashindano hayo itapelekea kuwepo kwa umoja na mshikamano pia kuhamasisha
wanadu toka maeneo tofauti kuwachangia wanafunzi ambao wanasoma katika mazingira
magumu chuoni hapo ili kuwawezesha kumalizi vizuri masomo yao.
Michuano hiyo
itajumuisha timu mbali mbali za vyuo vyote toka mkoani Iringa.
Chapisha Maoni