Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amefunguliwa
mashitaka na FA, Chama cha Soka England, kwa
utovu wa nidhamu.
Maneno ambayo yanaweza kumsulubu Mourinho
yalitolewa Jumamosi mara baada ya Chelsea
kuchapwa 3-1 na Southampton kwenye Mechi ya
Ligi Kuu England iliyochezwa Uwanjani Stamford
Bridge.
FA imedai maneno ya Mourinho yanamaanisha
Marefa wanapendelea na hivyo ni kinyume cha
Sheria.
Kwenye Mechi hiyo na Southampton Mourinho
alichukizwa na Refa Robert Madley kuwanyima
Penati na kudai Marefa huogopa kuwapa Chelsea
Penati.
Mourinho, mwenye Miaka 52, amepewa hadi
Alhamisi Oktoba 8 Saa 2 Usiku kwa Saa za
Tanzania, kujibu mashitaka hayo.
Hiyo Jumamosi, mara baada ya kutoa kauli yake,
Mourinho pia alitabiri FA itamfungulia mashitaka.
Licha ya kusakamwa na vipigo Vinne katika
Mechi 8 za Ligi Kuu England ambayo wao ndio
Mabingwa na kutupwa Nafasi ya 16 wakiwa
Pointi 10 nyuma ya Vinara Man City, Klabu ya
Chelsea Jana ilisema bado wana imani na
Mourinho.
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Related Posts
- Anonymous25 Nov 2016GERRARD HATA KAMA TUPO AFRIKA TUTAKUKUMBUKA DAIMA, KISOKA
Gwiji wa Liverpool, Steven Gerrard amestaafu rasmi kutumikia mchezo wa Soka ikiwa ni baada...
- Anonymous15 Jun 2016RATIBA LIGI KUU YA UINGEREZA 2016/17 HII HAPA
EPL August 13/14 Arsenal v Liverpool Bournemouth v Manchester United Burnley v Swa...
- Anonymous12 May 2016TIMU ZILIZOSHUKA DARAJA UINGEREZA HIZI HAPA
Klabu ya Norwich City imeshushwa daraja kutoka Ligi ya Premia licha ya kuandikisha ushindi dhidi ya ...
- Anonymous05 May 2016BOSI WA LEICESTER CITY AMWAGA MAGARI YA KIFAHARI KWA WWCHEZAJI
Mercedes B-Class Electric Drive. Thamani yake ni pauni £32,670 (zaidi ya Sh million 103) kwa g...
- Anonymous06 Apr 2016UEFA CHAMPIONZ LIGI ROBO FAINALI
Mechi zote kuanza Saa 3 Dakika 45 Usiku Jumatano Aprili 6 Paris St-Germain v Manchester City ...
- Anonymous29 Mar 2016MOURINHO KUIJENGA UNITED
Meneja wa zamani wa Chelsea, Jose Mourinho anadaiwa kuanza kujipanga na Manchester United kama atac...
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni