Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Beki wa kimataifa wa Ujerumani, Mats Hummels ametangaza hana nia ya kujiunga na magwiji wa ligi Premier Uingereza, Manchester United na atachezea Borussia Dortmund musimu ujao.
Kulingana na taarifa za jarida la Kicker, Alhamisi, Hummels, 26, amekataa kukubali mwito wa majitu hao wa Uingereza United kwa kudhibitisha atatii kandarasi yake na Dortmund inayoisha 2017.
 
“Ni haki kutosha kwa Mats kupatia ombi hilo wazo lakini nimesisitiza amekuwa mipangoni yetu kwa kina,” mkurugenzi wa michezo wa Dortmund, Michael Zorc alisema.
Alibaini kuwa alikutana na nahodha wa timu hiyo Hummels na babake Hermann ambaye ni wakala wake ambapo waliafikiana “wazi” atabakia na Dortmund.
Vyombo vya habari Uingereza vilitangaza United walikuwa wamewasilisha ombi la pauni milioni 40 kumnasua kutoka Dortmund ambao mwalimu wao maarufu, Jurgen Klopp anaondoka.
Nyota huyo wa Ujerumani atakuwa na jukumu kubwa kujenga upya miamba hao ambao wamedorora pakubwa musimu huu licha ya kufika fainali ya kombe la Pokal.


Chapisha Maoni