Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.








Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka (TFF), inatarajiwa kukutana jumapili tarehe 24, Mei mwaka huu ikiwa ni kikao cha kawaida cha kamati hiyo.


Moja ya ajenda katika kikao hicho itakua ni kupokea na kujadili mienendo, maandalizi na maendeleo ya timu zetu za Taifa za mpira wa miguu nchini.
Taarifa za ndani za TFF zimeeleza pia kutakuwa na mjadala kuhusiana na utendaji wa Kocha Mart Nooij wa Taifa Stars.

Stars imeonekana kutokuwa na mwenendo mzuri chini ya Kocha huyo Mholanzi.

Mfano mzuri ni michuano ya Cosafa ambako tayari imecheza mechi mbili na kufungwa zote.

Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajia kurejea Dar es salaam usiku wa kesho Ijumaa mara baada ya kumaliza mechi yake ya kukamilisha ratiba dhidi ya Lesotho itakayopigwa kesho kuanzia majira ya saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika masharik


Chapisha Maoni