Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Leo nimeamua kuleta part 3 ya story yangu. Hii ni kwasababu kaka yangu Kola Adebayor na ndugu zangu wameamua kuzungumzia mambo ya familia kwenye social media, kutuma baria kwenda kwenye club na radio. Ningeweza kuandika kitabu na kuuza lakini nimeamua ku-share na wewe hapa.
Miaka 25 iliyopita kaka yangu mkubwa Kola alienda ujerumani na kuwa tumaini kubwa kwa familia yetu. Wote tuliamini angeweza kubadilisha maisha ya familia yetu. Miaka baada ya yeye kuondoka Togo bado hatukua na umeme wala simu, Kama angetaka kuongea na sisi alikua anapiga simu kwenye hotel inaitwa Atlantic Hotel ambayo ilikua karibu na nyumbani kwetu.
Nilivyopata nafasi ya kwenda kucheza mpira France kwa mara ya kwanza, tuliitaji pesa kwa ajili ya ticket ya ndege na gharama nyingine. Kaka yangu hakupatikana kusaidia katika hili, mungu pekee anajua alichokua anakifanya huko Ujerumani.
Nilivyofika Ujerumani nilijaza makaratasi yote na timu ikaniruhusu kukaa kwenye academy. Baada ya miezi michache Kola akataka kunitembelea, nilikua nakaribia kuishiwa na pesa na nilikua naishi kwenye academy. Kwa hiyo nikaamua kuazima pesa ili kulipia hotel yake. Wakati huo mchezaji mwenzangu Sega N’diaye kutoka Cameroon alikua na pesa za kutosha akaniazima pesa. Pia ikabidi niazime pesa zaidi ili niweze kumpa Kola atumie kwenye safari yake ya kurudi Ujerumani.
Baada ya miaka michache mambo yakaanza kwenda vizuri, nashukuru mungu nikasaini mkataba na Mets.Tangu siku hiyo kaka yangu alikua anawasiliana na mimi muda wote ukifika muda wa kulipia bili zake za mwezi.Kuna muda alikua anasema kwamba mwanae anaumwa, so ikabidi nizoee tu
Nikawa na bahati zaidi ya kupata ofa kutoka Monaco na nikasaini mkataba nao. SIku moja Kola na marehemu Peter walikuja kunitembelea Monaco. Kaka zangu hawa wawili hawakuniambia kama walikua wanakuja. Lakini damu nzito kuliko maji nikawapokea. Walifika asubui sana mimi nikiwa naelekea kwenye mazoezi.Nilivyorudi tulikua na mazungumzo na walisema wanataka kuanzisha biashara ya magari. Ki ukweli biashara hiyo inahusisha pesa nyingi sana lakini niliwambia nitawasaidia nikipata malipo yanayofuata.
Wakati huo Thierry Mangwa alikua anaishi kwenye nyumba yangu kwasababu alikua ana matatizo binafsi so ikabidi tukae wote.Siku moja narudi kutoka mazoezini nikamkuta analina na hajawai kuniambia kwamba hata kaka zangu hawakuniambia.Siku nyingine rafiki yangu Padjoe alikuja kunitembelea na wakati anaondoka nikampa €500. Kaka yangu Kola alivyojua hivto alikasirika sana. Alikua hajaelewa kwanini nimpe rafiki pesa na sio yeye. Sababu ilikua ni simple, pesa aliyokua anataka Kola ilikua ni nyingi.
Siku moja nilikua nimechoka sana baada ya mazoezi nikaamua kulala, nilivyoamka nikakuta kisu shingoni mwangu na kaka zangu walikua wanapiga kelele kwamba nawapotezea muda.Nikawauliza hii ndio njia ya ku-solve tatizo, basi niueni na mchukue pesa. Basi wakaniacha na kuweka kisu chini.
Mama akanishauri niite polisi na nikafanya hivyo lakini damu nzito kuliko maji nikaacha yapite.
Baada ya mwezi nikarudi Togo nikashangaa mama yangu akibwatukia kwanini nimewaita polisi kisa kaka zangu wakati yeye ndie aliyenishauri hivyo. Akasema mimi ni mtu mbaya kwenye familia.
Kila muda nikirudi Togo watu wananiuliza kwanini kaka yangu Kola harudi kutembelea nyumbani baada ya miaka yote aliyoenda Ujerumani.Nikamnunulia ticket ya ndege na kumsafirisha hadi nyumbani kwa gharama zangu mwenyewe.

April 22, 2005 baba yetu alifariki na kabla ya hapo aliniambia nihakikishe msiba wake usiwe sehemu ya masikitiko bali tufurahie na kujivunia maisha yake hapa duniani. Mimi nikanunua ticket kwa ajili ya kaka zangu wote na tukaenda Togo na nikafanya kama baba alivyoseama.Kola anaejiita baba wa familia alifanya nini kwenye huo msiba licha ya kukaa ujerumani miaka yote.


Chapisha Maoni