Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kocha wa Uhispania Vicente de Bosque
amemuacha nje mshambuliaji wa timu hiyo
Diego Costa kwa mechi mbili za kufuzu kwa
michuano ya mabingwa Ulaya mwaka ujao.
Costa anahudumia marufuku ya mechi moja kwa
kupata kadi nyingi za njano na alikuwa hawezi
kucheza mechi ya kwanza dhidi ya Luxembourg
mnamo tarehe 9 mwezi Octoba.
Del Bosque:Tumeona tusimshirikishe kwa mechi
ya pili dhidi ya Ukraine.
''Hachezi vibaya'',Del Bosque alisema kuhusu
Costa,na kuongezea kwamba Uhispania
itamshirikisha katika mechi za usoni iwapo kila
kitu kitakwenda sawa.
Costa pia anahudumia marafuku ya mechi tatu
nchini Uingereza kwa kusababisha ghasia katika
ushindi wa Chelsea dhidi ya Arsenal baada ya
kuweka mikono yake katika uso wa mlinzi
Laurent Koscielny.
''Sikupendelea kile nilichokiona'',Del Bosque
alisema kuhusu kisa hicho.''Sipendelei kile Costa
alichokifanya''.



Chapisha Maoni