Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Mchezaji mmoja nchini Uingereza
amefungwa jela mwaka mmoja kwa kosa la
kumvunja mguu mchezaji wa klabu pinzani kwa
kumkanyaga mara kadha wakati wa mechi.
Nathaniel Kerr, 24, alikiri mashtaka mbele ya
hakimu katika mahakama mjini Manchester,
Uingereza.
Mchezaji aliyeumizwa Stuart Parsons, 30, alikuwa
akijibizana na mmoja wa mchezaji mwenzake
Kerr kwenye mechi ya ligi ya Sunday muda mfupi
kabla ya kisa hicho uwanjani katika eneo la
Stockport.
Kerr alimkanyaga Parsons mara kadha hadi mguu
wake ukavunjika na ilimbidi kufanyiwa upasuaji
na kukaa wiki kadha hospitalini.
Parsons alipokuwa amelala uwanjani akiwa na
maumivu tele, Kerr alimwambia mwenzake kwa
sauti: “Nimefanya haya kwa ajili yako”
Konstebo wa polisi Louise Spencer, wa kikosi cha
polisi cha eneo kubwa la Mancheste, alisema:
"Jeraha hili lilimwathiri sana mwathiriwa, na
hakuweza kufanya kazi wala kusaidia familia
yake change.
"Alilazimika kutegemea hisani ya wachezaji
wenzake waliolazimika kufanya michango kukidhi
mahitaji yake ya kifedha.
"Wakati huo wote, Kerr hajaonyesha majuto
yoyote.”
Alisema kukamatwa na kuadhibiwa kwa Kerr ni
ishara kwamba “uhuni na ujambazi” katika mechi
za kandanda hautavumiliwa tena.



Chapisha Maoni