Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kikosi cha timu ya Taifa ya
Tanzania (Taifa Stars)
inayodhaminiwa na bia ya
Kilimanjaro Premium Lager
kimeanza mazoezi leo mchana
katika uwanja wa Taifa
kujiandaa na mchezo dhdi ya
Malawi utakaocheza Jumatano
Oktoba 7, 2015 kuwania
kufuzu kwa Fainali za Kombe
la Dunia mwaka 2018 nchini
Urusi.
Stars inayonolewa na kocha
mkuu mzawa Charles Mkwasa,
akisaidiwa na Hemed
Morroco, Peter Manyika na
mshauri wa Ufundi Abdallah
Kibadeni wameingia kambini
jana katika hoteli ya Urban
Rose iliyopo Kisutu jijini
Dar es Salaam.
Wachezaji wote wameripoti
kambini isipokuwa wachezaji
wa kimataifa wanaocheza
soka la kulipwa nje ya
nchi, Mrisho Ngasa, Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu
wanaotarajiwa kuungana na
wenzao mwishoni mwa wiki
baada ya kumaliza michezo
inayowakabili wikiendi hii.
Wachezaji waliopo kambini
ni magolikipa All Mustafa,
Aishi Manula, Said Mohamed,
walinzi Juma Abdul, Shomari
Kapombe, Mohamed Hussein,
Haji Mwinyi, Hassan
Isihaka, Kelvin Yondani na
nahodha Nadir Haroub
“Cannavaro”.
Wengine ni viungo Himid
Mao, Mudathir Yahya, Frank
Domayo, Said Ndemla, Salum
Telela, Deus Kaseke, Saimon
Msuva, Farid Musa,
washambuliaji John Bocco,
Rashid Mandawa na Ibrahim
Hajibu



Chapisha Maoni