Na alex Mapunda,Jelamba viwanjani.
kuendesha mpira wa miguu kwa kuzingatia sheria kumi na saba za soka
ili kuepuka mivutano na matukio ya kuwapiga waamuzi yasiyokuwa ya
lazima yanayotokea mara kwa mara viwanjani.
Akizungumza na Jelamba Viwanjani mwamzi mkongwe wa soka toka Iringa
bwana Kasanga Kasanga amesema mara nyingi waamuzi wanabebeshwa mzigo
na lawama kubwa katika matukio ya soka yanayotokea uwanjani ambapo
mwamuzi akipuliza firimbi viongozi wanadhani amewakandamiza kwa
kutokujua sheria 17 za soka suala ambalo linasababisha waamuzi kupigwa
au kutishiwa viwanjani.
''sisi waamuzi tunapata shida tunapokuwa uwanjani kwa kuwa asilimia
kubwa ya viongozi wa timu zetu hawajui sheria na kanuni za mpira kitu
ambacho kinahatarisha uwezo na maamuzi yetu sisi kwa kuwa mara nyingi
maamuzi yetu uwanjani yanalalamikiwa na viongozi wa timu mbali mbali
licha ya kutumia sheria ya soka kitu ambacho endapo kitafumbiwa macho
soka letu litazidi kurudi nyuma,alisema kasanga.
Mara kwa mara kumekuwa na matokeo ya waamuzi kulalamikiwa hapa nchini
kutokana na matukio yasiyokuwa ya kiungwa yanayotea viwanjani ambapo
mara nyingi wahusika wamekuwa wakitupiana mpira huku kila mmoja
hakimnyoshea kidole mwenzake kuwa ndiye sababu ya kuharibu mpira wa
miguu hapa nchini.
Chapisha Maoni