Hamis Mtepa
TAREHE31-03-2014.
Katika orodha ya wachezaji mahili waliowai tokea
katika nafasi ya goli kipa kwa soka la hapa nchini Hamis
mtepa ni miongoni mwao, ambaye aliwika akiwa na Tenesco ya songea pamoja
na Maji Maji na kujizolea umaarufu mkubwa kwa uwezo wake mkubwa wa
kurinda lango.
Mtepa mzaliwa wa Mtwara huku Mnazi Mmoja[Lindu] alianza
kusakata kandanda katika shule ya msingi songea zamani ikifahamika kwa jina la
majengo ambapo nyota yake ilizidi kung’aa Zaidi alipojiunga na timu ya mtaani ya
Olimbiki Rangers mwaka 1984 wakati bado akiwa mdogo.
Baada ya kuitimu elimu ya shule ya
msingi mtepa alijiunga na masomo ya sekondari katika shule ya luwiko songea
mjini lakini kwa bahati mbaya alikatisha masomo kwa matatizo ya kifamilia
ambapo akatimkia Mtwara, akiwa huko alikiputa na timu ya ushirika ya
mtwara timu ambayo akuchezea kwa muda mrefu akasajiliwa na timu ya
kiwanda cha misitu mafinga ambako aliitumikia kwa msimu mmoja na mnamo mwaka
1988 alitua Tanesco ya songea hapo ndipo kipaji chake kilionekana baada ya
kufanikiwa kuipandisha timu hiyo toka ligi daraja la Tatu adi ligi kuu kipindi
kile ligi daraja la kwanza.
Mwaka 1993 kwa mara ya kwanza
alicheza mechi chache za ligi kuuu akiwa na Tanesco lakini baadae
ilitokea stofahamu ambapo Mkurugenzi wa Tanesco Simon Mwavile aliwasimamisha
wachezaji wote wa Tanesco kucheza mpira na akawapa onjo kali na kuwaambia
asiyetaka kufanya kazi Tanesco akacheze mpira, basi timu ikavurugika na ukawa
mwisho wa kucheza ligi kuu.
Baada ya seke seke hilo yeye,Amburosi
pamoja na Mbopa Luoga walisajiliwa na timu ya Soka ya Maji Maji,kipindi hicho
Wanalizombe walikuwa na kipa Shaibu Kambanga pekee ambapo walikuwa
wakimwitaji sana Mtepa kutokana na umahili wake wa kuringa lango lakini kitu
ambacho kilitokea baada ya kucheza mechi mbili za nyumbani Tanesco walimzuia
kusafiri na Maji Maji na wakamwamishia Mtwara kikazi ili kumkomesha.
Akiwa Mtwara mwaka 1994 Tanesco
walimruhusu kuchezea Taifa cup akiwa na timu ya Mkoa wa Mtwara ambapo
alichezea adi mwisho wa mashindano ,kufikia mwaka 1997 sheria ndani ya Tanesco
zilipungua makali baada ya kutokea mabadiliko ya utawala hapo akarudishwa
songea na akasajiliwa na Maji Maji suala ambalo lilimpa faraja kubwa sana
ambapo alikitumikia kikosi hicho adi mwaka 2006.
Je?unafahamu baada ya mwaka 2006 alienda wapi?pia jumatano
atasimulia jinsi alivyozuiwa kucheza Bandari mtwara na Tanesco.
Chapisha Maoni