Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Na Sophia Mwaipyana,Mbeya.
TAREHE 06-04-2014.


Displaying g.JPG


Timu ya Mbeya City ni timu ambayo imepanda daraja nakuleta changamoto kubwa kwa timu kubwa hapa nchini  ambapo ilifanikiwa kumaliza mzunguko wa kwanza bila kupoteza mchezo wowote.

Musa mapunda ndiye mwenyekiti wa timu ya Mbeya City  toka mwaka timu hiyo ilipo anzishwa Jelamba Viwanjani imefanya maojiana naye na akatuelezea machache kuhusu timu hiyo

“mimi ni  mwenyekiti wa Mbeya City, katibu wangu Emmanuel Kimbe na mwalimu Juma Mwambusi na Maka  kocha msaidizi”

“timu ilianza ikiwa na wachezaji 25 na tulipo panda daraja mwaka 2013 tuliongeza wachezaji wachache,ambapo wengi wao niwale walio ipandisha timu daraja”

Katika lengo la kuendeleza michezo katika mkoa wetu mgurugenzi wa jiji la Mbeya aliyekuwa kipindi hicho Juma Eddy na meya Atanasi Kapunga ndiyo walitoa wazo hilo na kupendekeza kuazishwa kwa timu ya Mbeya City .

Bahati nzuri  pendekezo hilo lilipitishwa hivyo timu ya Mbeya City waanzilishi wake ni jiji ndiyo maana timu hiyo inamilikiwa na  jiji chini ya baraza la madiwani  na maitaji yote tunapata kutoka katika bajeti iliyo tegwa na jiji ukiachia mbali wadhamini wa ligi kuu voda na Azam.

Siri ya mafanikio yenu nini

“kikubwa  timu yetu tuna wachezaji wanao jitambua na wanatambua wajibu wao kwa  timu  ,kwani wachezaji wanao jituma  na wanao jitolea kwajili ya timu,kwa kweli ni wachezaji wenye uzalendo na timu yao”

“pia mwalimu mzuri,ushirikiano wa wachezaji na mwalimu pamoja na viongozi,pia kuungwa mkono na mashabiki wetu ambao wamekuwa nyuma yetu kila wakati ”


Mmejipanga vipi  kuhakikisha ili kuhakikisha timu inasonga mbele?

“lengo letu kubwa ni kufika mbali  na kikubwa ni kupindua utawala wa simba na yanga

Nikweli kuwa mnapendwa sana kuliko timu ya Prisons

“sina uwakika sana kwani sisi siyo kwamba tunamashabiki wengi Mbeya peke yake hapana kila mkoa tuna mashabiki,ikitoka Simba na Yanga basi timu yetu inafuata kwa kuwa na mashabiki wengi”

“tuna mashabiki wengi kwasababu tuna fanya vizuri sidhani kama tungekuwa tuna fanya vibaya kama watu wange wangetupenda lakini kwa sababu tunafanya vizuri na tunamushirikiano mzuri na mashabikiwetu ndiyo maana tuna mashabiki wengi”............................................................................................................................................

endelea kumakinika na JELAMBA VIWANJANI jumanne wiki hii utaendelea kufahamu mengi kuhusu mbeya City.



Chapisha Maoni