Stivin Mapunda Garrincha wapili toka kushoto,mchezaji wa zamani wa simba,maji maji na Timu ya taifa stars.
“Sababu ya mimi kugombana na
mwenyekiti wa Fat Mhidin Ndolanga chanzo ni kocha wa timu ya Taifa kipindi hicho,
ambaye pia alikuwa kocha wa timu ya prisons ya mbeya Charles Boniface mkwasa
kuwapanga wachezaji wa timu yake ya Prisons katika mechi ngumu nchini Rwanda
kati yetu na Rwanga kwa kuwapa uzoefu wachezaji wake ili wafanye vizuri ligi
kuu bara,na kuwaacha wachezaji muhimu nikiwemo mimi, ambao tulikuwa wachezaji wazuri.
“Wakati mechi ikiendelea Ndolanga
alimtuma mjumbe wake kuja kumuuliza kocha kwa nini mapunda hajaaza katika
kikosi cha kwanza?,kocha alikaa kimya baadae akajibu ataingia,wakati huo hata
wachezaji wezangu benjini walimwambia mapunda inatakiwa aingie akaokoe timu kwa
kuwa tayari tulikuwa tumeshafungwa goli 1 hata hivyo kocha hakuchukua maamzi
yoyote.
“Lakini zikiwa zimebaki dakika tano
mpira kumalizika Mkwasa akaniita kwa Hasira nikapashe ili niingie nikaamua
kukataa kwa kuwa muda ulikuwa umeisha hali hiyo ilimkasirisha na akaamua
kuandika ripoti ya jumla kuhusu mechi hile kuwa Mapunda alikataa kucheza tangu
mwanzoni mwa mchezo, ali ambayo ilimfanya mwenyekiti wa Fat akasilike na kusema
kuwa Sitacheza timu ya Taifa hadi hatakapo ng’atuka madarakani.
“Ugomvi wetu ulikuwa mkubwa hadi
ukasababisha waziri Juma kapuya kumfungia Ndolanga kutokana na vurugu ambazo
zilifanyika mara kwa mara kwa wadau na mashabiki wakishinikiza nicheze
mpira,lakini mara baada ya Ndolanga kurudi Madarakani na kukaa kiti kimoja
kuzungumzia mgogoro wetu na yeye kujua Tatizo, mambo yote yakaisha na hadi hivi
sasa mimi na Ndolanga ni Marafiki wa kudumu.
Itaendelea…………..
Endelea kufuatilia
ambapo kesho tarehe 14 mwenzi 4 atasimulia kuhusu timu ya jeshi ya Botswana na
simba itakuwaje? Uskose kusoma jelamba viwanjani.
Chapisha Maoni