ENDELEA KUFUATILIA
HISTORIA YA STIVIN MAPUNDA GARRINCHA AMBAPO JANA ALIISHIA KUSIMULIA, MGOGORO KATI
YAKE NA MWENYEKITI WA FAT KIPINDI KILE SONGA NAE.
Garrincha wapili toka kushoto walioinama.
MECHI NINAYOIKUMBUKA
“Naikumbuka sana mechi ya Clab
bingwa kati yetu Simba na Timu ya jeshi toka Botswana,mwaka2003 ili kuwa mechi
muhimu kwetu na tulicheza katika kipindi kigumu ambapo wachezaji 5 muhimu wa simba
walikuwa wamefungiwa na mimi nilipewa jukumu la ukepteni,mechi ambayo ilichezwa
uwanja wa TaifA jijini Dar es salam,mechi tulipata ushindi dakika ya 89 ya mchezo bao
ambalo liliwekwa kimiani na mimi mwenyewe baada ya kubanwa sana na wapinzani
wetu.
“Watu wengi wakizani kwamba mechi ya
marudiano Tutatolewa kutokana na ushindi mwembamba ambao tuliupata nyumbani
lakini mambo yakawa tofauti, tukiwa ugenini tulicheza kwa morali kubwa na
tukafanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0,na tukafanikiwa kusonga mbele amapo
mechi iliyofuata tulipambana na Zamareck ya Misri mchezo ambao tulipata ushindi.
Mchezaji ninayempenda kwa sasa.
“Wachezaji wengi wanacheza vizuri
lakini mtanzania anayekipiga Tp Mazembe nchini kongo Mbwana Samatta, nampenda
sana ni mchezaji ambaye anatambua cha kufanya pindi awapo uwanjani.
Beki aliyekuwa anamsumbua
“kiukweli mabeki walikuwa
wananiogopa,mara nyingi nilikuwa nakabwa na mabeki wane,watatu, kwa kuwa
nilikuwa mtu hatari sana ,mabeki wote nilikuwa nawaweza.
Ushauri wake kwa Timu ya Maji Maji.
“Viongozi wazieshimu pesa za club,na
waakikishe wanapigana hili kupata pesa za kuendeleza timu,kwa ajili ya maji
maji.
“Hivi karibuni maji maji inatarajia
kufanya uchaguzi wa viongozi wapya,ni wakati wa wanachama kuinusulu club ya
Maji Mji kwa kuchagua viongozi wasio na uchu wa kutumia pesa za timu kinyume na
Makubaliano.
Maisha Baada ya Soka
“Hivi sasa nimeoa na nina mke na
watoto 3 na umri wangu ni miaka 36,namshukuru mwenyezi mungu kutonana na soka
nafahamiana na watu wengi ambao wengi wao tunasaidiana katika maisha kiukweli
mpira umenifungulia dira ya mafanikio yangu.
“Nina ofisi na najishugulisha na
ukandarasi wa majengo pamoja na bara bara,lakini nafikiria kuwa na ofisi kubwa
ili kuhakikisha najijenga vizuri zaidi kimaisha.
Zawadi kwa Watanzania.
“Nina mpango wa kujenga shule ya
soka ‘sports academy centre’ambayo itafundisha mpira kuanzia ngazi ya chini ili
kuwapata wachezaji wenye uwezo wa hali ya juu wa kucheza soka hapa nchini.
“Natarajia baada ya muda mfupi
ujenzi utaanza kwa kuwa tayari taratibu za awali zimeshakamili na shule hiyo
natarajia kujenga mkoani Ruvuma.alisema Garrincha.
Mwisho
Endelea kufuatilia
mfurulizo wa makala za wachezaji AMBAPO WAMESTAAFU SOKA wa hapa Nchini
waliowika nje na ndani ya TANZANIA.
Chapisha Maoni