Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Na Sophia Mwaipyana,Mbeya

Kocha wa timu ya Tukuyu Stars Jocia Stephano  asema  timu yao ya sasa hainasapoti  kama ilivyo kuwa Tukuyu stars ya kipindi cha nyuma hali inayo sababisha wafanye vibaya na kupoteza matumaini ya kurudi ligi kuu tena.

Timu hiyo ambayo kwasasa inashiriki ligi ya mkoa na ilifanikiwa kutinga katika atua ya sita bora,ambayo ikinolewa na Stephano aliyeanza kukinoa kikosi hicho mwezi wakwanza  baada ya kumpokea Charles Makwaza katika mzunguko wa pili.

 Stephano alisema kuwa kwasasa timu haina mfadhiri kwaahiyo kila kitu tunajitegemea wenyewe tuwachangishe wachezaji ilikuweza kujipatia maitaji madogomadogo kama usafiri ,maji.

“unakuta tunacheza tukiwa katika kipindi kigumu sana kwahiyo lazima  timu ishindwe kufanya vizuri kama watu wanavyo tarajia sababu timu ilikiuwa najina kubwa sana na ilikuwa inafanya vizuri sana”

“timu ya Tukuyu Stars kwasasa  haipewi sapoti na mtuyoyote Yule kuanzia wilayani hadi kwa wananchi wenyewe kwahiyo tunaangaika  viongozi  tuu”

“mimi nauwakika timu hii tukipewa sapoti kuanzi kwa wananchi hadi wilayani naimania baada ya miaka kadhaa ile timu ya Tukuyu Stars itarudi kama miaka  ya nyuma”
Mwisho  


Chapisha Maoni