RECODS
Manchester
United wana rekodi ya kushinda mechi 6 za mwisho walizocheza na timu
kutoka Bundesliga na rekodi yao ya kiujumla dhidi ya timu za kijerumani
wanapocheza Old Trafford - wameshinda mara 8, safe 3 na wamepoteza mechi
2. Rekodi yao ya ugenini na nyumbani ipo hivi ushindi mechi 14, sare 7
na kufungwa 6.
Bayern
wanasaka ushindi wa tano mfululizo katika ardhi ya UK. Msimu huu
walishinda 3-1 dhidi ya Man City katika makundi na wakaifunga 2-0
Arsenal katika hatua ya 16 bora. Msimu uliopita, walishinda 301 dhidi ya
Arsenal katika hatua ya 16 bora kabla ya kurudi England katika dimba la
Wembley kuwamaliza wajerumani wenzao 2-1 katika Fainali ya UCL.
Rekodi ya Bayern dhidi ya timu za kiingereza ipo hivi W16 D15 L12.
Bayern hawajapoteza mechi msimu huu - Je United itavunja mwiko huu?
Barcelona vs Atletico Madrid
Barca
wameingia kwenye Champions League wakiwa ni moja ya interesting team.
Ila kwa performance yao ilivyo mwaka huu, ni ngumu kusema moja kwa moja
kuwa ni favourite, japokuwa chochote kinaweza kutokea ukichukua
reference mwaka 2009 na 2011.
Baada
ya kuwatoa Man City kwenye raundi iliyopita, timu ambayo Barca walikuwa
wakiihofia zaidi kukutana nayo ni Bayern Munich, wamepata draw against
Atletico Madrid timu ambayo inaonesha kuwasumbua zaidi Barca recently na
sasa wanachuana vikali kwenye top position ya La liga wa msimu huu,
Atletico hawajapoteza mechi yoyote dhidi ya Barca (wamepata draw tatu)
hali ambayo inawapa extra confidence kwa maana wanaweza ku progress to
semi finals kama watapata draw mbili ambazo zitawa favour na away goals,
pia wachezaji hatari wa Atletico kama Diego Costa na Koke wanaongeza
confidence kuwa watashinda dhidi ya Barcelona.
Lakini
ikumbukwe kwamba hapa tunaongelea Barca, bingwa mara 3 kombe hili, pia
wana kikosi imara na chenye uzoefu wa kufanya lolote lile ndani ya dk
90, hapa bila shaka huwezi kuacha kulitaja jina la Lionel Messi ambaye
ana rekodi ya kuifunga Atletico Madrid magoli mengi kuliko timu nyingine
yeyote.
RECODS
FC
Barcelona wana rekodi ya kushinda mara 4 na kufungwa mara 5 katika
mechi 9 dhidi ya timu za Hispania katika michuano ya UEFA. Pia
walipoteza fainali ya mwaka 2006 ya UEFA Super Cup kwa kipigo cha 3-0
kwa Sevilla FC in Monaco.
Atlético
hawajawahi kufika kwenye hatua hii katika michuano ya UCL tang msimu wa
1996/97 walipofungwa na AFC Ajax. Rekodi ya Atletico katika robo
fainali ni ushindi wa me chi 3 na wamefungwa mara 2 kutoka katika robo
fainali 5.
Chapisha Maoni