KELVIN Haule ni miongoni viungo washambuliaji wachache ambao walikuwa na uwezo mkubwa wa kufunga ambapo jina lake lilikuwa kubwa alipochezea Tukuyu Stars, Maji Maji Pamoja na Timu ya Taifa “Taifa Stars”.
Katika mAzungumzo maalum na JELAMBA VIWANJANI ameeleza mengi kuhusu maisha yake
ya soka wakati akicheza
“nilianza kucheza soka Tangu nilipokuwa mdogo kwa kuwa niliupenda mchezo huo,lakini nilianza kucheza soka la ushindani katika kiwanda cha nyuzi Iringa mwaka 1983,hapo nilicheza kwa kipindi cha mwaka 1 na mwaka 1984 nilijiunga na timu ya Reli ya Iringa hapo nilicheza kwa mafanikio makubwa baadae nikasajiliwa na timu ya Tukuyu stars [Mbeya]ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara, kwa sasa Ligi kuu ya vodacom.
“nilianza kucheza soka Tangu nilipokuwa mdogo kwa kuwa niliupenda mchezo huo,lakini nilianza kucheza soka la ushindani katika kiwanda cha nyuzi Iringa mwaka 1983,hapo nilicheza kwa kipindi cha mwaka 1 na mwaka 1984 nilijiunga na timu ya Reli ya Iringa hapo nilicheza kwa mafanikio makubwa baadae nikasajiliwa na timu ya Tukuyu stars [Mbeya]ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja la kwanza Tanzania bara, kwa sasa Ligi kuu ya vodacom.
“nilisakata kabumbu kwa kipindi cha miaka mitatu nikiwa na Tukuyu stars,ambapo timu yetu ilifanikiwa kushiriki michuano ya Afrika mashariki mara baadaa ya timu yetu kufanya vizuri na katika michuano hiyo tulifanikiwa kufika hatua ya robo fainali na bahati mbaya tulitolewa na Sports Club Villa toka Uganda katika mechi ambayo tulifungwa goli 4-1 na tukaaga mashindano.
“kwa kipindi chote ambapo nilikuwa na Tukuyu Stars nyota yangu iling’aa sana ambapo timu mbali mbali zilikuwa zikinigombania lakini mwaka 1987 nikaamu kujiunga na Maji Maji ya songea maarufu kama wanalizombe na hapo nikacheza kwa mafanikio makubwa zaidi na nikaiwezesha maji maji kuwa mabingwa wa ligi ya muungano mara ya tatu,mwaka 98 na kupata nafasi ya kushiriki klabu bingwa afrika chini ya Meneja wa mahili wa maji maji wa kipindi hicho Shaffy Bora.
“ Maji maji nilicheza kwa kipindi kirefu kutokana na uongozi mzuri na mshikamano ambao ulikuwepo ndani ya timu hiyo na kufikia mwaka 2000 nikaondoka,na kwa kipindi chote hicho kuanzia mwaka 1987 – 2000 nilipata nafasi ya kucheza timu ya taifa ambapo wakati huo kiwango changu kilikua zaidi na nikafahamika nje ya mipaka ya Tanzania na umaarufu wangu ukaongezeka mara dufu.
“Niliamua kutundika daruga rasmi mwaka 2002 nikiwa na miaka 39 nikiwa na Twiga Stars ya kinondoni timu ambayo sikucheza kwa mafaniko makubwa kutokana na kwenda kwa umri na kutofurahishwa na maslahi ya kipindi hicho hapo nikatundika daruga na kubakia katka timu za veterans.
SIMBA, YANGA WANAANGAMIZA VIPAJI.
“Sikucheza timu kubwa kwa sasabu timu hizo toka kipindi hicho hazikuwa na malengo endelevu kwa wachezaji kikubwa walikuwa wanaitaji uduma ya mchezaji na sio kumjengea mchezaji maisha ya baadae,lakini nikacheza kwa mafanikio makubwa ingwa sikujiunga na timu hizo ambazo zina mizengwe na zinawajali wachezaji wa upande.
“Kuna kipindi nilitekekezwa na Yanga hotelini mwaka 1987 wakati nipo na Yukuyu Stars kwa kipindi cha mwenzi mmoja bila kujua hatima yangu ni ipi huku wakinipa matumaini ya kunipa mkataba lakini tulishindana baadae kwa kuwa Yanga waligoma kuniamishia kikazi jijini Dar es salam na wakanitaka nicheze bila kazi kwa kuwa kipindi kile kila Timu ililazimika kumtafuta mchezaji kazi nje ya soka nikaamu kuachana nao na na kujiunga na Wanalizombe mjini Songea.
itaendelea kesho tarehe 16-4-2014' atasimulia tukio la kuvunjika mguu,,,,,,,,,,,,
Chapisha Maoni