Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Ilipoishia……….
“nalikumbuka bao ambalo nililifunga  mwaka 1998 nikiwa na Timu ya Maji Maji ya Songea dhidi ya wekundu wa msimbazi Simba Toka Jijini Dar Es Salam, mara baada ya Kelvin Haule kuingiza crosi safi Toka winga ya kulia nami Sikufanya hajizi nikapiga shuti kali golini ambapo kilichotokea hata mimi sielewi niliupigaje ule mpira Golikipa Joseph Katuba akiwa amezubaa Pale Golini ule mpira Uligonga mara tatu mwamba wa juu na chini kwenye chaki mfurulizo…….
Itaendelea endelea kufuatilia mfurulizo wa makala haya kila siku Jelamba viwanjani

DAVID MJANJA WAPILI TOKA KUSHOTO WALIOSIMAMA
songa nayo......

 na kutumbukia Kimiani,ni tukio la pekee ambayo mimi sikumbuki kama limewai tokea katika mechi zingine.


Mechi anayokumbuka

“Kipindi nipo yanga ilikuja timu toka afrika kusini [ Vall professional] ,ilikuwa mechi ngumu sana nakumbuka ilikuwa club bingwa Afrika raundi ya kwanza na mimi niliingia kipindi cha pili na katika mechi hiyo tulifanikiwa kupata ushindi wa bao 2-1,hali ambayo ilipelekea mchezo wa marudiano kuwa mgumu zaidi kwani ilitulazimu kusafiri hadi ugenini.

“Hatukukata tamaa  tukafanya mazoezi ya nguvu na tukajiweka fiti kwa ajiri ya mchezo wa marudiano,katka mchezo huo wa marudiano ambao ulichezwa nchini afrika kusini tulicheza kwa kujituma sana na hadi mwisho wa mchezo tuliambulia sare ya bao 1-1,ambapo bao la ugenini likatusogeza katika raundi ya pili ambayo tulipambana na timu kutoka visiwa vya usheli sheli.


Hakuwai humia


“Mungu mweza wa yote kwani kwa kipindi chote ambacho nilikuwa nikicheza kwa takribani miaka 15,sikuwai humia nilikuwa nacheza mpira bila matatizo yeyote zaidi tuu ya maumivu ya kawaida pindi mchezaji atokapo uwanjani kama ilivyokuwa kwa wachezaji wezangu.


Maoni yake kuhusu Timu ya taifa

“Timu ya taifa ya sasa imepiga hatua angalau wachezaji wanacheza mpira wa kuvutia ila kinachotakiwa kufanyika ni wachezaji kuwa wazalendo pamoja na Tff kuwa karibu Na timu kwa hali na mali.


Baada ya kustaafu

“kwa sasa mimi ni Askari Magereza kazi ambayo niliipata tangu nilipokuwa nikichezea Tanzania Prisons mara baada ya kuwapa masharti ya kuto kuchezea timu yao hadi watakapo nipa kazi kweli walilidhia ombi langu na wakanifanyia mpango wa ajira ya kudumu.

“Sasa ivi nipo Singida ambapo Nimeoa na nimna watoto wawili,pia nafanya kazi ya ufundi ambao niliusomea kabla ya kuanza kungara katka medani ya Soka.
Anasimulia David Mjanja ambaye kwa sasa yupo bize na kazi ya uaskari magereza amapo kwa kipindi chote ambacho amecheza mpira alipata nafasi ya kuchezea timu ya taifa mara moja tu katika mechi ya kirafiki zidi ya Kenya wakati yupo Ushirika ya Moshi,pia amekili wazi kuwa alikuwa akisumbuliwa sana na Mohamed Mwameja wa Simba ambaye katika maisha yake ya soka alifanikiwa kumfunga bao moja pekee.

mwisho



Chapisha Maoni