Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




 
SHAIBU KAMBANGA MLINDA MLANGO WA ZAMANI WA MAJI MAJI

ILIPOISHIA JANA……………………..


  ''Asilimia 90 ya viongozi wa Maji Maji ni mashabiki na wadau wa Simba hadi hivi sasa hali ambayo inapelekea Maji Maji kufungwa Nyumbani na ugenini huku wakijikakamua  sana ni sare mara nyingi simba inapofika Songea toka miaka ya 1990,maandalizi yanakuwa afifu sana na tatizo kubwa ni ushabiki wa viongozi
.
SONGA NAYO………………


  ''Mara nyingi mechi na  yanga maandalizi yanakuwa makubwa sana ndani na nje ya uwanja na ukizingatia viongozi wengi ni wanachama wa Simba,MAJI MAJI huingia uwanjani kwa lengo moja tu  kuiangamiza yanga,kiukweli kwa kipindi cha miaka ya hivi karibuni ushindi kwa Yanga katika uwanja wa Maji Maji ni sare.



  ''Lakini tatizo kubwa ambalo limepelekea Maji Maji kuwa na Hasira kubwa kwa Yanga kuna wakati Maji Maji iliposhuka daraja kwa Mara ya Kwanza mchezo wa Mwisho walikutana na Yanga kila timu ilikuwa ikiitaji pointi moja tu kwa maji maji asishuke  Daraja lakini kwa Yanga kutangazwa bingwa.


  ''kitu ambacho kilitokea katika mchezo ule ambao  nakumbuka ulipigwa Morogoro Yanga waliisaliti Maji Maji na kuishindilia  bao 4-0,hali ile ilipelekea uhasama na Yanga kuongezeka mara dufu na toka siku hiyo adi leo Yanga hawajawai pata ushindi Songea.

 Ardhi Wameninyang'anya uwanja wangu.



   ''wakati nacheza  Maji Maji timu ilinipa viwanja Viwili kimoja ENEO la Ruvuma kingine Msamala,lakini kitu ambacho kimetokea ardhi wamenipora na nimejaribu kufuatili hakuna ufumbuzi uliopatikana hali ambayo inanipa uchungu mkubwa Sana nikikumbuka huwa najawa na hasira kali sana.

  ''Lakini nashukuru uwanja wa Ruvuma nimejenga na upo vizuri na maisha yanazidi kusonga.


Malanzi ya tambazi yamezorotesha Maisha yangu.



  ''Mwaka huu toka mwenzi wa saba sijafanya kazi,kutokana na mguu wangu kuvimba sana kwa homa ya  Tambazi.  



Kwa asiyefahamu tambazi ni uvimbe ambao unatokea sehemu yeyote ya mwili unafafanana na jipu lakini kwa tambazi uvimbe unakuwa mkubwa sasa kwa sisi waafrika unaweza kusema umerogwa,kumbe ni mkusajiko wa sumu pamoja na uchafu ambao unakuwa umejikusanya sehemu moja ya mwili na unatafuta sehemu ya kutokea.

  ''kwa kweli mguu wangu ulikuwa umejaa sana hali ambayo ilipelekea kuacha shughuli zote na kushinda nyumbani, huku mke wangu,pamoja na boss wangu wa kampuni ya Ottawa wamekuwa wakiniudumia vizuri sana mungu awape baraka tele,na naendelea vizuri nitarejea kazini kama dereva muda sio mrefu.


Mchezaji anayempenda.

  ''Wachezaji wengi wanapewa Majina makubwa ambayo yanapingana na uwezo wao lakini Mrisho alfan Ngassa namkubari sana kwa kufanikiwa kuzichanganya Simba,Azam na Yanga na kwasasa ametajirika kupitia timu hizo.

Ushauri kwa Maji Maji.



Viongozi wa Maji Maji wameweka wigo mkubwa kwa wachezaji wa zamani, Sisi ndio tunajua mbinu mbali mbali za kimpira na tunajua  timu inatakiwa kufanya nini ikiwa katika wakati wowote bila kujali pesa,watupe nafsi ya kuwa karibu na  timu naamini tutatoa mchango Mzuri.

 ''Kuna kipindi Mlale Jkt walinichukua wakati wanakaribia kupanda daraja niliwashauri mambo mengi sana adi leo wanaeshimu mchango wangu.

Anachokumbuka akiwa mchezaji Wa  Maji Maji.

  ''kuna kipindi mbinu za mwalimu zinakuwa zimefeli uwanjani inalazimika kutumia nguvu za ziada ili kupata ushindi sisi Maji Maji tulikuwa na mtu alikuwa anaitwa Evans Ponella huyo alikuwa balaa kwa kumiliki mpira na kupiga chenga mimi namfananisha na J J Okocha wa Nigeria,basi ikifikia dakika ya 80 timu imefungwa au tunaitaji ushindi,wachezaji wote tulikuwa tukipeana ishara kuwa pasi zote ziende kwa ponella.

  ''Yeye Alikuwa na stamina ya hali ya juu na alikuwa akikata chenga kuelekea eneo la 18 kutokana na uwezo wake alikuwa anawauzi sana mabeka na wakawa wanamfanyia sana faulo hali ambayo ilipelekea sisi kupata penalti nyingi sana na mara nyingi tulikuwa tunaibuka na ushindi dakika za mwisho kupitia yeye.

Baada ya kustaafu mpira.

  ''Mimi ni dereva,nimeendesha magari ya serikali,taxi na sasa ni dereva wa Basi katika kampuni ya Ottawa high Class safari za kwenda dar,maisha yangu yanaenda vinzuri.

  ''Ninamke na watoto 3 nilizaliwa mwaka 1966 naipenda sana familia yangu,Anaitimisha Shaibu Kamba kwa kushusha pumzi ndefu mara baada ya kusimuli matukio mazito ambayo hakupenda kuyakumbuka kwa kipindi hiki.  

…………………………………………………mwisho………………………………………………………..
 USIKOSE KUSOMA JELAMBA VIWANJANI KWA MAKALA NYINGINE NYINGI ZA WACHEZAJI WA ZAMANI.


Chapisha Maoni