JOHN KABISA MCHEZAJI WA ZAMANI WA MAJI MAJI YA SONGEA |
Ilipoishia,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
“mwaka 1979 tulicheza mechi ya kirafiki kati ya RTC na Yanga katika mechi ile nilipigwa kichwa cha makusudi hadi kuzimia na mchezaji wa Yanga Hamad Omari akitokea nyuma yangu na baada ya tukio hilo yanga wakamtoa nje na kumwingiza mchezaji mwingine.
“Tatizo ni kwamba tulipishana maneno ya kimpira na mimi milikuwa mwiba mkali kwa timu yake na yeye pia na hadi mwisho wa mchezo tulifungwa bao 1-0,kwa tukio lile siwezi kumsahau kwa kuwa ilikuwa makusudi.
Endelea,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Ushirikina Michezoni.
“Mwaka 1985 kulikuwa na pambano kali kati ya maji maji na Pan Afrika pambano ambalo ilitakiwa lichezwe siku ya Jumamosi lakini pan walichelewa kufika uwanjani kwa sababu ambazo hazikuwekwa wazi na pambano likahailishwa adi siku ya Jumatatu.
“Kipindi hicho Maji Maji alikuwa imemuleta mzee wa kamati ya ufundi Toka Kigoma ambaye alikuwa anahakikisha kamati ya ufundi nje ya uwanja inakwenda sawa.
“Yule Mzee tulimpa jina la Mzee Mziba jina la mchezaji maarufu kutokea kigoma,kwa kweli mimi nilikuwa siamini imani hizo lakini yule mzee nilimweshimu sana,nakumbuka alituambia kwa kuwa mechi yenu na Pan itachezwa siku ya Jumatatu mtashinda bao 3-0,na hata kama mkipata nafasi nyingine ya kufunga bao haitawezekana.
“kwa kipindi kile Pan Afrika likikuwa Tishio Mimi sikuafiki kama tungeweza kupata ushindi mkubwa kiasi kile lakini sisi tulikuja kuamini mara baada ya kumalizika ule mpambano ambapo tulishinda bao 3-0 kama alivyotuambia yule mzee hatukupata bao lingine.
“Mzee Mziba alikuwa akieshimika sana na Maji Maji alikuwa akisafiri na Timu kila ilikoenda kucheza na kila ambacho alikisema ndicho ambacho kilikuwa kinatokea kwa hali ile yule Mzee alipata umaarufu mkubwa sana.
“Hakuishia hapo Maji Maji ilisafiri kwenda dar kukiputa na wekundu wa Msimbazi Simba mwaka 1985 mchezo wa ligi kuu ambapo tuliweka kambi yetu katika chuo cha usafirishaji cha Mabibo Dar,baada ya Chakula cha jioni Mzee Mziba alitutembelea katika kambi yetu na akatukuta tupo katika hali ya uzuni sana akatuuliza kwanini mpo katika hali hiyo?.
“Tukamwambia tunaofu juu ya mchezo wa kesho,Mzee Mziba alicheka sana na kwa maneno ya Dharau hakatuambia mchezo wa kesho ni raisi na msiwe na wasi wasi tutashinda mechi ngumu tayari tumeshacheza,tukaenda kulala.
“Uwezi kuamini Siku ya mechi tulicheza mchezo mzuri Sana kama alivyosema yule mzee Simba walikuwa wakitafuta mpira kwa tochi na hadi dakika 90 za mchezo ulipomalizika Tuliivurumisha Simba bao 2-1,mabao ya Maji Maji yaliwekwa kimiani na Selestine Sikinde pamoja na madaraka Suleman kisha lile ya kufutia machozi la Simba nakumbuka lilifungwa na Zamoyoni Mogela.
“Lakini Mzee Mziba aliendelea kuimalisha ufundi nje ya uwanja ambapo tulikuwa tumebakisha mechi 8 ili ligi imalizike na mechi nyingi zilibaki kanda ya ziwa,Mzee wetu akatuambia msiwe na wasi wasi ila kati ya mechi 8 zilizobakia mtafungwa mechi moja tu ila sijui mechi gani.
“kweli baada ya maneno yale mechi ambayo ilifuata tulipambana na CDA ya Dodomo mechi ambayo tulifungwa bao 1-0,na kuanzia hapo hatukufungwa tena mechi nyingine hadi tukamaliza ligi,hapo nikakumbuka maneno ya yule mzee na kuamini uwezo wake.
“Baada ya msimu Kumalizika nakumbuka yule Mzee alituaga na akatuaambia ameitwa uarabuni kwaajiri ya kwenda kutoa tiba,ambapo toka alipoondoka yule mzee hakutokea tena mwingine kama yule,na mimi imani ya kuamini mpira nje ya uwanja ikatoweka.
Hayo ni yam zee mziba akiwa na maji maji, endelea kufuatilia kesho intaendelea,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Chapisha Maoni