Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



kipa wa zamani wa Maji maji ya songea SHAIBU KAMBANGA akiwa na mwandishi wa gazeti la michezo la  championi pamoja na jelamba viwanjani wakati wa maojiano maalum nyumbani kwake hivi karibuni.



ilipoishia…………………

 ''Nakumbuka baada ya mazoezi na mwalimu nilikuwa nikimwita Madaraka na kunifanyia mazoezi ya mashuti tukiwa pekee yetu,alikuwa anapiga kwenye eneo la penalti na nje ya 18 mara nyingi tulikuwa tunaweka mashuti 40,lakini kutokana na uwezo wangu kati ya mashuti 40 nilikuwa naweza kudaka au kupangua mashuti  35 huku nikiruhusu kuingia kwenye kamba mashuti 4 au 5 pekee hali ambayo ilinifanya niimalike zaidi pindi niwapo uwanja hapo ndipo jina la Shilton lilipotea
.
Songa nayo……………







Acheza mechi 30 peke yake bila msaidizi.



  ''Nikiwa na Maji Maji niliwai kucheza mchezo 30 peke yangu bila msaidizi kipindi hicho mlinda mlango katika timu nilibakia pekee yangu mara baada ya wezangu kuondoka, morali ya mchezo kwangu ilikuwa juu sana.

  ''Kuna kipindi nilikuwa nimeumia goti katika mchezo dhidi ya Ushirika ya Moshi ilinilazimu kucheza kwa kuwa timu ilikuwa haina mlinda mlango mwingine,nikapigwa sindano ya ganzi na kuingia uwanjani, katika mchezo huo tulipata ushindi wa bao 2-0,hadi mwisho wa msimu nikiwa mlangoni pekee yangu timu ilimaliza katika nafasi ya nne.



Ulevi,wanawake tatizo kwa wachezaji.



Wachezaji wetu lazima wajitambue  kwa kuwa athari za kuwa na wanawake na kunywa pombe zipo wazi kwa mchezaji zinapunguza nguvu kwa wachezaji hasa wa siku izi wamekuwa wakionekana katika viwanja vya starehe siku za mechi ngumu pasipo kujali afya zao kama wachezaji.



  ''Mimi kwa uzoefu  wangu nafahamu mchezaji akifanya mapenzi inachukua siku 3 kurudisha nguvu zake za kawaida,mchezaji ili acheze vizuri kwa kiwango chake inatakiwa asifanye mapenzi siku tatu kabla ya mchezo na kama atafanya siku moja kabla hawezi akacheza kwa kiwango chake.




  ''Mimi muda wote ambao nilicheza katika kiwango cha juu kiwango changu kilikuwa kile kile kwa kuwa nilikuwa nafuata sheria za kurinda afya nikiwa kama mchezaji,kuna kipindi  nilikaa Miezi mitatu bila kukutana na mke wangu lakini kwa wachezaji wa siku izi ni ngumu.  

Itaendelea kesho tarehe 05-05-2014 ambapo atasimulia jinsi imani za kishirikina zilivyoipoteza timu ya maji maji.


Chapisha Maoni