Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




ENDELEA KUFUATILIA MAKALA YA SULEIMAN KITUNDA,MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA NA KM KM YA VISIWANI ZANZIBAR PAMOJA NA TIMU YA TAIFA YA ZANZIBAR.

ILIPOISHIA

“alikuwepo Saidi kambi{marehemu},Hakibu shabani kibunda,Rashid Mandaje,Issa Athumani{Marehemu}pamoja na Saidi Zimbwe,Wengine ni Said Jaba,Kaililila Mausi,Suleman kitunda,Said Mwamba,Abeid Mziba pamoja na Deo Shundu.

SONGA NAYOO…………………………….

Kutokea kwa Mtaa wa Mabibo Sahara.

"Jina la sahara asili yake lilikuwa ni jina la timu ya gereza ya wahindi ni timu ambayo tulikuwa tukicheza nayo pindi nilipokuwa small kids ya Yanga,wakati nikiwa mdogo  nilikuwa nikilipenda sana jina la sahara kiasi kwamba nilikuwa nikiliandika kwenye vibao na kubandika katika maeneo mbali mbali hali hiyo ilipelekea  kuanzishwa kwa timu ya sahara sports club ya mabibo timu ambayo wametokea wachezaji wakubwa sana hapa nchini akiwemo shaban kado,jina la sahara bado lipo hadi hii leo ambapo mtaa unafahamika  kwa jina la Mabibo sahara eneo ambalo kwa sasa kuna shule ya magara na vitu vingine vya kijamii,lakini vijana wengi bado hawaamini kama mimi ndio mwadhirishi wa lile jina.

Ushirikina uwanjani.

"wakati nachezea Maji Bomu ya bagamoyo nilifungwa ilizi kwenye nywele ambayo ilitengenezwa kwa mwonekano kama wa Sigara  ambayo ilikuwa na maana ya kubeba timu yangu na kuifunika timu pinzani na mimi nilikuwa ni naodha wa timu   hiyo,nakumbuka tulicheza na Home Boys kongoe ambapo hadi mwisho wa mchezo tuliibuka na ushindi wa bao 5-4.

"pia tukio lingine nakumbuka nikiwa yanga nilienda kucheza ndondo,nakumbuka nilichukuliwa na timu ya Visija Rangers ambapo nilichukuliwa na mganga akachukua karatasi akaandika maandishi ya kiarabu na akabandika kwenye jenzi yangu yakiwa yameangalia mbele ili kuwachanganya mabeki wa timu pinzini, kweli siku ile nilicheza mpira  wa hali ya juu sana nikafanikiwa kufunga bao tatu dhidi ya Kongowe Boys na tukaibuka na ushindi wa bao 3-0,kiukweli uchawi bado upo viwanjani hata  siku hizi wanasahau kufanya maandalizi kitimu badala yake wanaegemea upande wa tunguli na kusahau kuwa tunguri ni nyongeza tu katika mpira.
 

Sababu za timu ya taifa ya zanzibar kufanya vibaya kimataifa.

"wachezaji wengi wa zanzibar wanacheza timu za bara hali ambayo inapelekea timu za kule kubakia na wachezaji wa kawaida,pia zanzibar ni tegemezi kwa kuwa sio manachama  wa fifa hali hiyo inachangia kudhoofisha soka la zanzibar.

Yanga walipigwa 6,wakatupiga 6 lakini  tukawapa kombe Maji maji.

“Mwaka 1998 katika ligi ya muungano toka visiwani kulikuwepo na timu ya Polisi,Mrandege pamoja na sisi KM KM ambapo bara waliwakilishwa na Yanga,Maji Maji pamoja Tanzania Prisons Wajela jela toka Mbeya mbapo mchezo wa kwanza tulivaana na Yanga uwanja wa Taifa jijini Dar es salam Yanga walitukung’uta bao 6-0 na kikubwa nakumbuka yanga tulikutana nao mara bada ya wao kufungwa bao 6-0 na Rajar Kasabulanka ya morocco katika ligi ya Afrika basi wakamalizia hasira kwetu.

“lakini katika mechi ya Marudiano Zanzibar tuliwashikia bendera yanga na hadi dakika 90 za mwamzi zilipokamilika tuliibuka kidedea kwa kuwabamiza yanga bao 2-1 ushindi ambao uliwauma sana yanga kwa kuwa yanga walikuwa wanaitaji ushindi ili kuchukua ubingwa wa muungano ambapo mara baada ya kupoteza mchezo ule Maji Maji walitawazwa mabingwa mwaka 1998 kwa kuwa waliwafunga Prisons ya Mbeya Bao 1-0 bao ambalo liliwekwa kimiani na Amri Saidi.



“nakumbuka kikosi cha Km km alikuwepo Said athumani,mrisho sadamu,abdallah Nasibu,Afidhi amada,Abudallh Shaban[nyumba]pamoja na Juma sheha wengine ni Issa Amen[dokta],mohamed Said [Tishi],Amen mshimu,mimi mwenye Kitunda bila kumsahau Nichoraus Williamu.



Nilibebwa kama mfalme mpwapwa.

“mwaka 2006 nilichukuliwa na Mh.Gorge Simba Chawene Mbunge wa kibakwe ambapo alinichua ili kufundisha kibakwe Fc timu ambayo mbunge alinikabindi madaraka ya kutafuta vijana toka ngazi ya vijiji na nilifanikiwa kupata viwanja wazuri sana ambapo timu yetu ilikuwa ikishiriki ligi daraja la nne mimi nikiwa kama kocha.



“Nakumbuka kuna mechi tulicheza na Mji Mpwapwa tukatoka nao Sare nakumbuka siku hiyo nilibebwa kama mfalme na wamabiki wa kibakwe Fc huku wakiimba kiukwili kutokana na kazi ambayo nilkuwa nikiwafanyia walikuwa wakinichukulia kama Nabii ambapo pia kuna baadhi ya wachezajia ambao niliwakuza na wakafanikiwa toka timu ile akiwemoShuhuri Dickson,Baraka  mfugale,Issaka Rongersgodfrey kimonga,jowabu madii, Malongotito,oska Madelemo pamoja nakiller gaitani.

Bao kali.

"wakati nipo yanga kuna mechi ilikuwa kati ya yanga na Kombaini ya Zanzibar basi siku hiyo nilichukua mpira nikawalamba chenga mabeki wa tatu wa zanzibar akabikia kipa pekee yake baada ya kuniona nipo mbele yake akaduwaa na kudondoka nikafunga bao kiraisi sana, sasa siku hiyo baba yangu alikuwepo uwanjani siku hiyo na hakuwa kunishuudia uwanjani nikicheza mpira kwa kiwango cha juu basi alishangilia sana adi mashabiki wa yanga wakamnyanyua juu huku wakiimba.

Maisha baada ya soka.

Nimeoa ninawatoto watu Mke wangu anaitwa Upendo,mimi ni kocha wa Makuburi United ligi daraja la tatu timu inafanya vizuri ,soka limenisaidia sana nina nyumba zanziabar pia ninajenga nyingine Dar es salam,kwa sasa ni mwajiliwa wa kampuni ambayo inausika na mambo ya ulinzi hapa dar na mke wangu anafanya kazi katika shule ya perfect division,anaitimisha sulemani Kitunda ambaye amewai kuitumikia timu ya Taifa ya Zanzibar mara Mbili mwaka 1996 pamoja na mwaka 1997,na kwa wadau wa soka anapatikana kwa namba zifuatazo,0716308568,0757667773.


Chapisha Maoni