Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





John Kabisama.


Ukiikumbuka Maji Maji ambayo ilikuwa inatikisa hapa nchini Miaka ya 1980 hadi 1990 uwezi kumweka kando John Kabisama ambaye alikuwa ni miongoni mwa viungo washambuliaji bora kuwai tokea katika timu Hiyo na Tanzania kwa ujumla.

Kabisama,mzaliwa wa Mbambabei Wilayani Nyasa alianza kusakata kabumbu katika Shule ya msingi Maji Maji zamani hikifahamika kama ‘Haideli’Songea Mjini.Amezungumza na Gazeti hili na kueleza mengi kuhusu Soka:


“Nilianza Kucheza soka la ushindani nikiwa na RTC ya Arusha mwaka 1977 ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja ya kwanza na nikiwa na timu hiyo nilipata bahati ya kuitwa kwenye timu ya taifa kutokana na umahili wangu wa uwanjani kwa mara ya kwanza na ya mwisho.


“Lakini mwaka 1978 nilijiunga na Kill Tex ya Arusha timu ambayo nilidumu nayo kwa misimu miwili ambapo baadae mwaka 1983 nikatimukia AICC pia ya arusha,timu ambayo niliichezea kwa mafanikio makubwa.


‘Mwaka 1885 Maji Maji ya Songea wakanichuka Toka AICC[timu ya ukumbi wa mikutano Arusha] kutokana na kiwango changu kuwa kikubwa sana nikiwa kama kiungo mshambuliaji ambapo kwa iliyewai kuniona nikicheza anavifahamu vitu vyangu, Maji Maji niliichezea kwa kwa mafanikio makubwa sana ambapo nikiwa na timu hiyo tulifanikiwa kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa mara mbili mfululizo,mwaka 1885,1986.

“Na mwaka 1989 baada ya kuona kuwa soka nimeshalitendea haki na kucheza kwa muda mrefu nikaamua kugeukia shughuli za kawaida,anasema Kabisama kisha anaendelea:

Ajira kikwazo timu kubwa.

“Wakati nipo RTC ya Arusha Yanga  na Pan Afrika walinichukua lakini tulilishindana kuhusu ajira wao walitaka nicheze mpira peke yake ingawa uwezo wa kunipa ajira walikuwa nao.


“Na kipindi kile kwa kuwa hapakuwa na ajira ya moja kwa moja katika timu tulikuwa tunategemea ajira ambayo timu inakutafutia hivyo mimi sikuwa tayari kujiunga na timu ambayo haikuwa tayari kunipa ajira nikaamua kurudi RTC ya Arusha.

Kutokea kwa kona za Maji Maji.

“ Mwaka 1987 Maji Maji tulienda nchini Zimbabwe kupambana na Power Diynamo katika Roundi ya kwanza ya Club Bingwa Afrika,nakumbuka mechi ile ilikuwa ngumu sana kwetu kwani tulifungwa bao 5-1 na bao letu lilifungwa na Abdullah Chuma.

“Mechi ya marudiano tulitakiwa kwenda Jijini mwanza ili kupambana na wapizani wetu,tulijiandaa vizuri ili kulipiza kisasi cha bao 5,lakini kilichitokea tulipata ajari mbaya sana wakati wa safari nyuma kidogo kabla ya kufika Madaba Toka Songea mjini,eneo ambalo lina kona nyingi sana ambapo kutokana na ajari ile eneo hilo hadi leo linaitwa kona za Maji Maji.

“chanzo cha ajari ile ni kwamba bosi wa basi ambalo tulitakiwa kwenda nalo mwanza alikorofishana na Dereva wake akaamua kuendesha mwenyewe,na kwa kuwa yeye alikuwa mgeni wa Bara Bara ya Songea hakuzifahamu zile kona hivyo baada ya kuzipita kona kadhaa alifikiria zemeisha ,kufumba na kufumbua tukajikuta tupo nje ya Bara Bara.

“Katika ajari ile wote Tulipona ila mimi nilikatika karibia nusu ya ulimi pamoja na maeneo ya miguu nilijisikia maumivu makali sana,lakini mtu ambaye aliumia sana nakumbuka ni Mweshimiwa Joel Bendera mkuu wa mkoa wa morogoro ambaye alikuwa mwalimu wetu lakini mungu alimsaidia baada ya wiki mbili akapata nafuu.

“Tukashindwa kwenda mwanza wenzetu wakapata ushindi wa mezani licha ya sisi tulipata ajari,maamzi yale mimi binafsi yaliniuma sana kwa kuwa nilikuwa na hasira sana na wale jamaa toka Zimbabwe.

Hawezi kusahau

“mwaka 1979 tulicheza mechi ya kirafiki kati ya RTC na Yanga katika mechi ile nilipigwa kichwa cha makusudi hadi kuzimia na mchezaji wa Yanga Hamad Omari akitokea nyuma yangu na baada ya tukio hilo yanga wakamtoa nje na kumwingiza mchezaji mwingine.

“Tatizo ni kwamba tulipishana maneno ya kimpira na mimi milikuwa mwiba mkali kwa timu yake na yeye pia na hadi mwisho wa mchezo tulifungwa bao 1-0,kwa tukio lile siwezi kumsahau kwa kuwa ilikuwa makusudi.

itaendelea ambapo kesho tarehe 12, john kabisama atasimulia kuhusu ushirikina michezoni na jinsi maji maji walivyomsajili mzee mziba toka kigoma.


Chapisha Maoni