Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


stasahau tulipigwa viboko Tanga na mashabiki wa coastal union,mechi ikavunjika dakika ya nne






Haji Mambo.

Ukizungumzia Timu ya soka ya Lipuli Fc ya mkoani  Iringa lazima utamtaja  Beki mahili wa kipindi hicho Haji Mambo ambaye aliwika na  timu hiyo miaka ya 1998 hadi 2002 kwa mafanikio makubwa.

Mambo alianza kusakata kandanda toka akiwa mdogo katika shule ya msingi Azimio, Iringa Mjini  na kiwango chake kiliongezeka mara dufu katika michuano ya umiseta taifa yaliyofanyika zanzibar na shinyanga mwaka 1991 pamoja na 1992 kipindi icho akiwa mwanafunzi katika sekondari ya ruaha.

aliokuwa sekondari pia alikuwa akichezea timu ya vijana afrika timu ya mtaani kabla ya kujiunga na African wonderers mwaka 1994  timu ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja la pili,mwaka 1994 alisajiliwa lipuli lakini aliamua kuondoka baada ya kumpiga chenga katika fedha za usajili na akatimkia magereza  ambayo alishezea kwa misimu miwili na mnamo mwaka 1998 akamwaga wino rasmi  Lipuli Fc baada ya kufanyika makubariano mazuri.

Mambo alicheza lipuli kwa moyo na mafanikio mkubwa lakini mwaka 2000 akatimkia Jkt mapotopola ya dodoma ambapo walimwaidi kazi lakini ndoto zake zikayeyuka baada ya kuumia nyama za paja na ikashindikana kuingia jeshini, akarudi  Lipuli na kaitumika kwa msimu mmoja na hatimaye mwaka 2002 akaachana na soka la ushindini kwa muda ingawa  alikuwa na kiwango cha hali ya juu.

Baada ya kuachana na lipuli alianzisha timu yake ya watoto wadogo timu ambayo iliundwa na wachezaji wenye vipaji na timu  ilipata nafsi ya kushiriki ligi ya mkoa,lakini haikusonga mbele kutokana na matatizo mengi ya wazi ya kisoka yanayolikabiri soka la Iringa ikiwembo viongozi kupendelea baadhi ya timu.

Mwaka 2008 wadau wengi wa soka walimshauri kurudi uwanjani ili kuongezea nguvu timu ya polisi iringa suala ambalo alilipokea kwa mikono miwili jiunga ambapo akiwa na polisi alichaguliwa  kutumikia timu ya mkoa ya Iringa katika mashindano ya Taifa cup na  walitolewa na timu ya mkoa wa mbeya katika hatua ya robo fainali ambapo mwisho wa michuano hiyo timu ya mbeya waliibuka mabingwa,na ndani ya mwaka huo akatangaza kuachana kabisa na soka,ni sehemu ya hisoria ya  Haji Mambo kisha anaendelea kueleza zaidi:-    

Stasahau

''wakati nikiwa lipuli mara nyingi tulikuwa tukicheza kwa kujitolea hasa mechi za nje ya iringa, nakumbua tulienda shinyanga kucheza na polisi shinyanga  tuliingia kwenye ofisi ya meneja wetu na kuiba mipira mitatu ya timu, baada ya kukosa nauli ya kurudi iringa.

"nilikuwa mimi Said Athumani pamoja na Kesi chombo ambapo baada ya kuiba mipira ya timu yetu tuliuza na tukapanda treini na kutoroka kuelekea iringa huku tukiwaacha wenzetu wakisota shinyanga.

"tulisafiri kwa traini bila kulipa fedha adi dodoma na wakati wa safari tulikuwa tukiama toka kwenye behewa moja hadi lingine ili kukwepa kuripa nauli na tukaingia Dodoma salama ambapo tukaenda kulala kwa ndugu yangu ambaye anaishi dodoma.

"siku ya pili safari ya kurudi iringa ikaanza na tulisafiri kwa basi la Kingcross basi ambalo mara nyingi timu ya lipuli ilikuwa ikitumia bure na sisi baada ya kujieleza tulipanda bure hadi iringa.

"nakumbuka zile fedha ambazo tuligawana baada ya kuuza mipira ya  timu tulianza kutumia baada ya kuwasiri iringa lakini wenzetu walikaa shinyanga kwa kipindi cha wiki moja kutokana na ukata ambao uliikumba lipuli.

Tulipigwa viboko Tanga.


"lipuli tulienda Tanga kucheza na  costal union ya Tanga tulipigwa sana viboko na mashabiki wa coastal union  hali ambayo ilipelekea  mechi hiyo kuvunjika dakika ya nne.

"kitu ambacho kilitokea ni kwamba mechi ya kwanza coastal walikuja Iringa na mechi iliisha vizuri lakini timu ya coastal baada ya kurudi tanga waliwaambia mashabiki wao kuwa walipigwa  wakiwa iringa suala ambalo waliwadanganya mashabiki wao na wakapanga kuripa kisasi.

''kweli kabla ya mechi kuanza walianza kutupiga kwenye benchi na baada ya kuona hilo wachezaji tukagoma kuingia uwanjani na dakika ya nne mwamzi akavunja pambano,uwezi kuamini mwandishi sisi tulitolewa uwanjani kwa ulinzi mkali kama waanga wa kivita na tulisindikizwa toka Tanga Mjini Hadi mheza na lengo kubwa lilikuwa ni kutuua kutokana na hasira ambazo walikuwa nazo.    
Baadhi ya wachezaji ambao waliumizwa ni pamoja na Shomari Abuchwaka,Joseph kanic,Idi tumaini pamoja Kesi chombo ambaye aliumia sana kuliko wote.

Tulitoka sare,tukatangazwa tumefungwa 2-0.

"nakumbuka tulienda kucheza na kaliakoo ya lindi nyumbani kwao mechi ilisha kwa sare ya bila kufungana tukapanda gari kurudi iringa tukiwa njiani jioni takasikiriza Radio Tanzania ikatoka habari kuwa tulifungwa na kaliakoo lindi bao  
2-0 tulishituka sana bila kuchelewa tuliailisha safari ya iringa tukaelekea dar kwenda kudai haki yetu.

"lakini ilishindikana kutengua matokeo kwa kuwa shirikisho la mpira wa miguu kipindi kile fat lilikuwa likitambua lipoti ya kamisaa pekee yake na katika mechi ile ilisemekana kamisaa alichukua rushwa na hata ndani ya dakika 90 sisi tulipata bao 2 za wazi zikakataliwa na kikubwa kariakoo lini ilikuwa ikitumia kila haina ya mbinu ili kuepuka mkasi wa kushuka daraja,vile vile walianza kututoa mchezoni kabla ya mpira kuanza ambapo mwamzi alitoa kadi nne za njano kwa George mketo,gwafika kiwanga,jabil mohamee na saidi chitalula bila kosa lolote.

Ushirikina uwanjani

"ulikuwepo,upo na utaendelea kuwepo, kuna kipindi lipuli tukuwa na mechi katika uwanja wa samora dhidi ya yanga na tulitakiwa kupata ushindi ilikujiweka katika mazinga mazuri ya kufuzu katika kinyang'anyiro cha michuano ya mungano.

"lipuli tulienda karenga karibu na makaburi usiku kufanyiwa tambiko na maganga wa jadi na siku ya mechi tuliiwafunga yanga bao 1-0 matokeo ambayo kwa  yanga  yalikuwa machungu kwa vile kama wangeshinda wangekuwa mabingwa.

"pia kingine ninachokikumbuka kuhusiana na mechi hiyo tuliingia uwanjani huku tukiwa na hasira kubwa na yanga kwa kuwa katika mchezo wa kwanza dar tulifungwa bao 5-0 na kocha wa yanga aliwaraumu wachezaji wake kuwa walicheza chini ya kiwango kwa kutufunga bao chache na akawapa adhabu ya kuzunguka uwanja kwa kweli tukio lile lilituuma sana na tukahaidi kuripa kisasi.

Uongozi wa mpira Iringa ni sifuri.
“mimi sasa ivi najishughulisha na kilimo pamoja na biashara zangu nimeachana kabisa na soka kutokana na uozo uliopo katika mpira wa iringa,mpira unaendeshwa kwa ajili ya manufaa ya watu wachache pasipo kuangalia jinsi ya kuweka mkoa wetu katika ramani ya soka hapa nchini.

“mimi ninacheti cha ukocha nimewai kufundisha timu nyingi ikiwemo mshindo Fc pamoja na Silver Fc kwa mafanikio makubwa katika ligi ya mkoa lakini viongozi wa iringa baada ya kugundua ninapenda sana haki wakawa wananinyang’anya poindi makusudi na kunitafutia matatizo mengi ili timu yangu isifike mbali kwa makosa yasiyo na kichwa wala miguu pia viongozi wa iringa kuna kipindi walinifungia mienzi mitatu kujiusisha na soka la Iringa bila kuweka wazi makosa yangu lakini baadae wakanifungulia.

“mpira wa iringa unaendeshwa kienyeji sana mwaka Fulani waliniteua kuwa kocha wa kopa coca cola mimi nilifanya mchakato wa kuteua wachezaji 60 wenye vipaji na nikawaambia viongozi wangu kuwa wanitafutie walimu wengine ili kushirikiana kuteua wachezaji 25 wazuri,kilichotokea ni haibu tupu waliingia ofisini viongozi wachachea na wakateua majina wenyewe,wakakata majina 35 na siku ya pili wakanikabidhi majina yaliyosalia kwa ajili ya kuendelea na maadalizi kiukweli niliwashangaa sana kwa kuwa watu ambao waliofanya maamzi hayo hawana uelewa wowote na mpira nikaamua kujiuzuru ili kulinda heshima yangu.

Mchezaji anaempenda.


“mrisho mgasa amecheza katika kiwango kizuri kwa muda mrefu nampenda sana.
`
Ushauri kwa soka la iringa.
“uchaguzi ufanyike haraka sana soka la iringa limevamiwa kiasi kikubwa sana toka kwenye vilabu,na hata uongozi wa chama cha mkoa,miminimepata hasira hadi ikapelekea kuamia wilaya ya kilolo na kulipa soka kisogo kabisa muda mwingine nikikumbuka mpira wa iringa natamani kulia.

Baada ya kustaafu soka.
Sifuatilii  kabisa soka la hapa iringa licha ya kuwa na cheti cha ukocha,naishi wilaya mpya ya kilolo nafanya shughuli zangu za kawaida nina mke na watoto watatu anaitimisha Haji Mambo ambaye ilikuwa beki mahili wa lipuli timu ambayo ilikuwa ikifanya vizuri miaka ya 1990 hadi 2000.


Chapisha Maoni