Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Tukio la kudondoka kwa kocha wetu uwanjani gafla na kufariki dunia,Mzee heri Kila nikikumbuka natokwa na machozi.



Suleman Kitunda.

Suleman kitunda Simota maarufu kwa jina la supercontroll ni miongoni mwa wachezaji bora ambao Hama hakika tutaendelea kuwakumbuka kutokana na uwezo wao mzuri wa kusakata kandanda uwanjani ambao waliowai tokea hapa nchini katika Nafsi ya ushambuliaji kuanzia miaka ya 1980 adi 2006 na mashabiki wangi walikuwa wakifurahishwa sana na aina ya uchezaji wake.

Kitunda mzaliwa wa Magomeni eneo  la makanya Jijini Dar es sam alianza kusakata kandanda katika shule ya msingi ya Mburahati National Housing Dar kabla ya kujiunga na masomo ya sekondari katika shule ya Kahole Mjini Bagamoyo, ambapo wiki hii anafafanua mengi kuhusu maisha yake ya soka katika Maojiano maalum na Jelamba viwanjani:-

“kipaji changu kilianza kuonekana nikiwa na Yanga small Kids mwaka 1984 ambapo pale nilikutana na watu kama Tomas Kipede pamoja na Mfaume Athumani chini ya kocha wetu mahili Bady sareh, ambapo nilicheza adi mwaka 1987 nikajiunga na Maji Bomu ya Bagamoyo timu ambayo ilikuwa ikishiriki ligi daraja la pili mkoa wa Pwani nikiwa pale nilikuwa na wachezaji kama Beatus Kilinga,Hamis pamoja na Oska manteku ambao wakikuwa wakinitengenezea mipira, hata hivyo sikukaa sana  mwaka 1989 nilichukuliwa na timu ya kiwanda cha usafirishaji  cha NAT ambapo baada ya uwezo wangu wa kupachika mabao kuongezeka kwa kasi nikasajiliwa rasimi na timu ya wakubwa ya Yanga mwaka 1991.

“maskini wa mungu! Baada ya kujiunga na yanga nilishikwa na homa ya ajabu ya kuvimba mguu hali ambayo ilininyima usingi kwa kuwa sikupata nafsi ya kucheza katika mashindano licha ya mwanzo kupata nafsi ya kucheza mechi za kirafiki kabla ya kuwa mgonjwa.

“niliambua kwenda kwa mganga wa kienyeji bagamoyo kwenda kutibiwa ugonjwa ule kwa kuwa niliamini homa ile dawa sahihi ilikuwa ni dawa ya kienyeji kwa kuwa kuna mtu niligongana nae na baada ya kupona nilijiunga na timu ya bohari kuu ambayo ilikuwa ikipigania kupanda ligi kuu mara baada ya yanga kukatisha mkataba wangu kutokana na kuugua,ambapo timu hiyo ilikuwa chini ya kocha Bady Sareh ambaye awali alikuwa yanga, kwa bahati mbaya Timu ya bohari kuu ilishindwa kupanda na badala yake ikapanda timu ya Tiger toka Mbeya Pamoja na katavi Ranger na kikubwa kilichopelekea tusipande sababu kubwa ni timu ya katavi rangers ilikuwa na uwezo mkubwa wa kusakata Kandanda pia mchango wa Hasan Mwanakatu ambaye alikuwa kiongozi wa mpira alifanya kila jambo ili kuhakikisha timu yake inapanda daraja kwa kuwa alikuwa mwenyeji wa mpanda, pia ndani ya mwaka huo nilichaguliwa na timu ya mkoa wa Dar es salam Mzizima united na tulifanikiwa kuchukua kombe mwaka 1992.

“mwaka 1993 nilijiunga na kikwajuni ya Visiwani Zanzibar timu ambayo sikukaa sana nikatimukia KMKM  pia ya Zanzibar timu ya kikosi cha kuzuia magendo chini ya kocha mzee Heri ambapo katika timu hiyo niliajiliwa pia kama Askari ,kiukweli maisha ya Km Km yalikuwa mazuri na nilicheza mpira kwa kujituma sana hadi mwaka 2006 nilipojiunga na timu ya superargentina nikiwa kama kocha mchezaji timu ambayo makazi yake yalikuwepo katika  eneo la Unguja ukuu hata hivyo sikukaa  sana mwaka 2007 nikachukuliwa na Gwerelo horians timu zote mbili zilikuwa zikishiriki madaraja ya chini lakini nikiwa na Gwerelo nilifanikiwa kuibuka mfungaji bora ambapo niliweka kimiani bao 14 na hatimaye mwaka 2008 nikatundika darga,anasimulia Suleman kitunda kicha anaendelea:-

Penalti ilikatisha uhai wa kocha wetu.

"hakika maisha anapanga mungu,katika maisha yangu kila nukta nikikumbuka tukio la kocha wetu wa km km kufariki Dunia Gafla katika uwanja wa Mau Unguja kwa presa ya mchezo ni tukio ambalo lilikua la maajabu sana ambalo lilileta simanzi kwa wanasoka wengi hapa nchini.

''ilikuwa kati ya KM KM na Mrandege ya Zanzibar, kitu ambacho kilitokea
 timu yetu ilipata Penalti ambapo mchezaji  mwenzangu baada ya kupiga ikagonga mwamba kocha Mzee heri alipatwa na hasira huku akimtupia lawama mpigaji baadae akachukua maji na kunywa, baada ya kunywa maji alidondoka chini na hatimaye akakata roho kiukweli tukio lile kwangu mimi ilikuwa ni sawa na kuchoma sindano kwenye kidonda kwa kuwa mzee Heri akikuwa ni dira kwangu,mungu amweke mahari pema peponi!,Amen.

Mechi ya kimataifa.

"mara yangu ya kwanza kucheza mechi ya kimataifa ilikuwa kati ya yanga dhidi ya timu ya taifa ya india mchezo ambao kwa upande wangu ulikuwa mgumu kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza  Kwanza likini nakumbuka siku ile tulicheza kwa kuelewana sana na tulifanikiwa kuwafunga India kwa jumla ya bao 2-1bao zote zikiwekwa kimiani na Said mwamba kizota,na bao zote pasi za mwisho zilitoka kwangu nakumbuka siku iyo tunacheza na Timu ya Taifa ya India kikosi cha yanga kilikuwa kama ifuatavyo:-



“alikuwepo Saidi kambi{marehemu},Hakibu shabani kibunda,Rashid Mandaje,Issa Athumani{Marehemu}pamoja na Saidi Zimbwe,Wengine ni Said Jaba,Kaililila Mausi,Suleman kitunda,Said Mwamba,Abeid Mziba pamoja na Deo Shundu………………………………………………


Itaendelea,endelea lkufuatilia  makala za wachezaji wa zamani kila siku JELAMBA VIWANJANI.


Chapisha Maoni