Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Jumatano Novemba 25
KUNDI A
Malmö FF v Paris St Germaine
Shakhtar Donetsk v Real Madrid
KUNDI B
2000 CSKA v VfL Wolfsburg
Man United v PSV Eindhoven
KUNDI C
1800 FC Astana v Benfica
Atletico Madrid v Galatasaray
KUNDI D
Borussia Mönchengladbach v Sevilla
Juventus v Man Cit

WAKIWA kileleni mwa Kundi B la UEFA CHAMPIONZ LIGI, UCL, Manchester United wanahitaji ushindi kwenye Mechi yao hii na PSV Eindhoven Uwanjani Old Trafford ili wafuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 huku wakiwa na Mechi moja mkononi.
Lakini PSV, inayoongozwa na Kocha Phillip Cocu, ambae alikuwa Mchezaji chini ya Meneja wa Man United Louis van Gaal huko Barcelona, iliifunga Man United 2-1 katika Mechi ya kwanza huko Amsterdam.
Kuelekea Mechi hii:
Man United wanatinga kwenye Mechi hii wakiwa na morali baada ya kulishinda lile wimbi la Droo 3 za 0-0 Mwezi Oktoba na kufanikiwa kupachika Mabao katika Mechi zao 3 zilizopita huku Wachezaji wao Watano tofauti wakifunga katika Mechi hizo wakizibwaga CSKA Moscow 1-0, WBA 2-0 na Watford 2-1.
Katika Mechi yao ya mwisho Majuzi Jumamosi Man United waliyoifunga Watford kwenye Ligi Kuu England na kupanda hadi Nafasi ya Pili, mmoja wa Wafungaji wao alikuwa Memphis Depay ambaye pia ndie aliefungana Bao la Man United walipocheza na Timu yake ya zamani PSV.
PSV wanaingia Mechi hii ya Old Trafford wakiwa hawajashinda hata Mechi moja ya Kundi B la UCL ya Ugenini baada ya kufungwa na CSKA Moscow na Wolfsburg.
Kwenye Ligi yao huko Uholanzi, PSV wako Nafasi ya Pili baada ya Juzi Jumamosi kuongoza 1-0 walipocheza na Willem II na kutoka Sare 2-2.
Hali za Wachezaji:
Louis van Gaal Leo amepata afueni baada ya Kepteni wake Wayne Rooney, Anthony Martial na Marouane Fellaini wote kurejea mazoezini na wote kuwa fiti kwa ajili ya Mechi hii baada ya kuikosa Mechi ya Jumamosi na Watford.
Wachezaji wenye maumivu na kuwa na hatihati ni Bastian Schweinsteiger, Phil Jones, James Wilson na Ander Herrera wakati Majeruhi ni Michael Carrick, Valencia na Luke Shaw ambae alivunjwa Mguu mara mbili kwenye Mechi ya kwanza na PSV.
Kwa upande wa PSV, Hector Moreno, ambae ndie alimvunja Mguu Luke Shaw, yupo kwenye maumivu na huenda asiwepo pamoja na Maxime Lestienne na Simon Poulsen.
Kumbukumbu:
Man United ishacheza na PSV mara 5 tangu wakutane kwa mara ya kwanza 1984 walipokutana kwenye UEFA CUP na Man United kushinda 1-0 Uwanjani Old Trafford na kuibwaga PSV Jumla ya Bao 1-0 kwa Mechi 2 na kisha kucheza kwenye Kundi la UCL Msimu wa 2000/01 ambapo PSV wlishinda 3-1 kwao lakini Old Trafford Man United iliitwanga PSV Bao 3 kwa Bao za Teddy Sheringham, Paul Scholes na Dwight Yorke.
Hivyo katika mara mbili walizocheza Old Trafford Man United walishinda Mechi zote 2.
Mtu hatari:
Kwa PSV ni Luuk de Jong ambae ndie anaoongoza kufunga Mabao kwa Timu yake na pia Ligi ya Uholanzi, Eredivisie, Msimu huu akiwa na Bao 11 lakini kwenye UCL Msimu huu amefunga Bao 1 dhidi ya Wolfsburg.
VIKOSI VINATARAJIWA KUWA:
Man United: David de Gea , Matteo Darmian, Marcos Rojo, Chris Smalling ,
Daley Blind , Jesse Lingard , Juan Mata ,
Morgan Schneiderlin, Bastian Schweinsteiger, Ashley Young , Memphis Depay
PSV Eindhoven: Jeroen Zoet, Santiago Arias, Joshua Brenet, Jeffrey Bruma, Héctor Moreno, Andrés Guardado, Adam Maher, Davy Pröpper, Luuk de Jong, Jürgen Locadia, Luciano Narsingh
REFA: Pavel Kralovec [Czech Republic]



Chapisha Maoni