England yabanwa na Ecuador 2 - 2
Raheem Sterling ambaye huchezea kalbu Liverpool, alibanduliwa uwanjani kwa kadi nyekundu katika dakika ya 11 baada ya mtafaruku kati yake na Antonio Valencia ambaye huchezea klabu ya Machester United.
Sterling amepigwa marufuku kushiriki mechi ya kirafiki itakayofuata.
Ecuador iliikanda kanda England na kutumia fursa ya ulinzi mbovu huku ambapo Enner Valencia aliwaongoza kushambulia awali lakini Wayne Rooney akapata fursa ya kupenyeza bao lake la 39 kufaidi England kabla ya kwenda mapumziko.
Sasa England itabidi kujipiga msasa wakijiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Honduras siku ya Jumamozi kabl aya kusafiri kwenda Brazil kuanza ngoma ya kupigania kombe la dunia.
Kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wafuatao ambapo kwenye mabano ni timu ambazo wanacheza:
Walinda mlango ni, Fraser Forster (Celtic), Ben Foster (West Bromwich Albion), Joe Hart (Manchester City).
Walinzi ni pamoja na, Leighton Baines (Everton), Gary Cahill (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Glen Johnson (Liverpool), Phil Jones (Manchester United), Luke Shaw (Southampton), Chris Smalling (Manchester United).
Viungo wanaounda timu hiyo ni pamoja na, Ross Barkley (Everton), Steven Gerrard (Liverpool), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Southampton), Frank Lampard (Chelsea), James Milner (Manchester City), Alex Oxlade-Chamberlain (Arsenal), Raheem Sterling (Liverpool), Jack Wilshere (Arsenal).
Washambuliaji ni pamoja na, Rickie Lambert (Southampton), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Danny Welbeck (Manchester United).
Chapisha Maoni