Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Etoo anasema kwa maagizo ya daktari anapaswa kupumzika
Nahodha wa Cameroon Samuel Etoo ana uwezekano wa kukosa kuchezea nchi yake wikii hii jumatano ,ambapo watachuana na Croatia kwa sababu ya jeraha analouguza.
Etoo hajafanya mazoezi kwa siku mbili na kuna uwezekano wa kutopona wakati wa kuchezwa kwa mechi hiyo ya group A,Manaus
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 33 aliandika kauli hii kwenye mtandao wa twitter, " madaktari wana uhakika kuwa sitaweza kushiriki katika mechi hiyo kwa sababu ya jeraha la goti linalonisababishaia maumivu.”
Cameroon na Croatia wote walishindwa katika mechi zao na wanakabiliwa na tishio la kutimuliwa katika kinyang'anyiro cha kombe hilo la dunia.
Cameroon walicharazwa bao moja kwa nunge walipopatana na Mexico huku Brazil wakiwafunga Croatia mabao matatu kwa moja.
Kukosekana kwa Etoo katika kikosi itakuwa pigo kubwa kwa Cameroon ambao walishindwa na Mexico hivyo basi inawalazimu kujikaza ili wasibanduliwe dimbani.
Etoo aliyepata jeraha la goti kwenye mguu wa kulia mwishoni mwa msimu wake katika kilabu cha Chelsea alisema anatumai kupata muujiza ili wweze kutetea ushindi wa nchi yake.
Aliongeza kwa kusema, " kama haitafayika hivyo,nitaendelea kutekeleza wajibu wangu kama nahodha ,hususan kama kaka mkubwa ili kuongoza wenzangu chipukizi kupata ushindi”
"Kwa muda wa miezi mitatu sijapata nafasi ya kupata nafuu hata kwa mechi za kukaribia kombe la dunia,sijaweza kufanya mazoezi kabambe hadi tulipopambana na Ujerumani katika mechi ya kirafiki.”
"Katika mechi dhidi ya Mexico,nilijaribu kwa uwezo wangu lakini baada ya kumuona daktari tuligundua nilihitaji mapumziko ,hata baada ya dakika ya tisa,nilikuwa nahisi uchungu.”


Chapisha Maoni