Maelfu waandamana kupinga kombe la dunia
Maelfu ya wenyeji wasio na makao
mjini Sao Paolo waliandamana nje ya uwanja utakaoandaa mechi ya kwanza
ya kombe la dunia alhamisi ijayo wakipinga gharama ya juu ya mashindano
hayo.
Maandamano hayo yaliwadia siku moja tu baada ya
rais wa Brazil Dilma Rousseff kuwahakikishia wageni na mashabiki wa
kandanda kuwa kamwe hatoruhusu maandamano yatie doa kwenye kipute hicho
cha kombe la dunia.Zaidi ya watu milioni moja waliandamana katika barabara za miji yote ya Brazil wakishinikiza serikali kupunguza ubadhirifu wa fedha na kupunguza matumizi yake kwa maandalizi ya kombe la dunia na yale ya Olimpiki yatakayofanyika mjini Rio mwaka wa 2016.
10,000 Waandamana kupinga Kombe la Dunia
Mapema wiki hii serikali iliwaongezea polisi wote mshahara ilikuzuia mgomo uliotishia kuporomosha hali ya utengamano huku fainali ya kombe la dunia likinukia.
Serikali imeahidi kutumia polisi na hata jeshi la taifa kudumisha amani na utengamano wakati wa kombe la dunia.
Chapisha Maoni