Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Ufaransa kuchuana na Nigeria


Valencia alioneshwa kadi nyekundu
Ufaransa ilikamilisha mechi za makundi kwa sare tasa dhidi ya Ecuador.
Licha ya sare hiyo Ufaransa ilisalia kileleni mwa kundi E ikiwa na alama 7 moja zaidi ya Switzerland iliyoisakama Iran katika mechi ya mwisho.
Les Blues wamefuzu katika raundi ya 16 bora ambapo sasa watachuana na Nigeria .
Ufaransa itachuana na Nigeria katika mkondo wa pili wa kombe la dunia.
 
Washindi wa kundi hilo Argentina watakuwa na kibarua kigumu dhidi ya Switzerland Jumanne ijayo katika uga wa Arena De Sao Paulo.


Chapisha Maoni