Rais wa shirikisho la soka
duniaFIFA Sepp Blatter ameyasifu mataifa madogo madogo kwa kuyaadhibu
mataifa ''makubwa''kisoka tena !
Blatter aliyasema hayo katika siku ya mapumziko kabla ya kuanzwa kwa mechi za robo fainali ya kombe la dunia huko Brazil.Aidha Hii pia ilifungua taswira ambapo timu 4 za bara Ulaya zilifuzu kwa mkondo huo wa robo fainali sawa na 4 kutoka mataifa ya Marekani kusini kinyume na matarajio ya wengi haswa baada ya kushuhudia mataifa yenye sifa kubwa katika kombe la dunia wakiwemo mabingwa wa dunia Uhispania ,mabingwa wa zamani Uingereza na Italia wakibanduliwa nje ya kipute hicho mapema katika raundi ya kwanza.
Mshindi katika mechi hiyo atachuana na mshindi kati ya wenyeji Brazil na Colombia.
Je kunauwezekano wa mataifa ya Marekani kusini kutawala kipute hicho huko Brazil ?
Hilo ndilo swali linalowasumbua wachambuzi wa makala haya ya kombe la dunia .
Majibu ya swali hilo yatapatikana jumamosi mwakilishi wa Marekani Kusini Argentina atakapokwaruzana na mwakilishi wa bara ulaya Ubeljiji.
Hatimaye mechi baina ya Costa Rica na washindi wa pili huko Afrika Kusini ,Uholanzi ndiyo itakayokamilisha vita vya ubingwa wa soka katia ya mabara hayo mawili.
Mataifa 4 ya Ulaya yatakabiliana na mataifa 4 ya Marekani Kusini
Hakuna taifa lolote la bara Ulaya ambalo limewahi kushinda kombe la dunia inapoandaliwa Kusini mwa Marekani.
Brazil ndilo taifa la pekee lililowahikutwaa ubingwa wa dunia katika kombe la dunia lililoandaliwa barani Ulaya.
Afrika na Asia na Oceania yamesalia kuwa mashabiki baada ya mataifa wakilishi kubanduliwa nje ya kombe hilo.
Je ni nani atakayeibuka kidedea Marekani kusini ama Ulaya.
Chapisha Maoni