Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




BONDI toka nchini Malawi Jonson Adam amewasili mjini songea mkoani Ruvuma tayari kwa  pambano la roundi 10 litakaofanyika tarehe 29 siku ya iddi dhidi ya bondia toka mkoani humo musa omari maarufu kwa jina la chitepete ambapo maandalizi ya mtanange huo yanaendelea vizuri na mgeni Rasimi atakuwa Francis cheka toka Morogoro.
 
Kulia ni bondia musa omari toka songea
Akizungumza na Championi Jumatatu Jonson adam alisema amejiandaa vizuri na pambano hilo ambapo licha ya kuja Tanzania kwa mara ya kwanza anamini ataibuka na ushindi kutoaka na maandalizi ambayo amejafanya.

“katika  rekodi yangu sijawai pigwa ila nimetoa sare mara mbili hivyo wanaruvuma na watanzania kwa ujumla wasitegemee mteremko nimekuja kufanya kazi na sio kucheza.

Vile vile mwalimu ambaye amekujanae mkoani Ruvuma Toka kyela mkoani mbeya ambao bondia huyo alifikia muddy Eliya alisema Jonson adam amekuja kufundisha ngumi hapa nchini ambapo musa kama ajajiandaa ajiandae kwani anaweza kufia uwanjani siku hiyo kwa kuwa Adam ni bondia mzuri.

Lakini kwa upande wake bondia toka Songea Musa omari  amewatoa hofu wanaruvuma na Tanzania kwa ujumla kwa kusema kuwa atahakikisha anamaliza pambano Roundi ya tatu kutokana na maandalizi ambayo amefanya na watu wa Malawi wajiandae kupokea msiba siku ya Iddi.

Mitanange mingine Itakayopigwa siku hiyo ni pamoja na jams Ntanga wa songea atakipiga na Furaha ndengenye toka Kyela pia Alibobu wa njombe ataonyeshana kazi na bondia toka songea,pia kutakuwepo na wasanii mbali mbali kama zimwi,linko pamoja na domo la mamba toka jijini Dar .
 
musa omari


Chapisha Maoni