WAKALI wa Tanzania Taifa stars leo wameshindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kurazimishwa na msumbiji sare ya bao 2-2 hatua ya mwisho ya mchujo kuelekea kupangwa
kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika
mwakani nchini Morocco.
katika mchezo huo Dakika 45 za kwanza zilimalizika bila bao na kipindi cha pili, Msumbiji walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 47 kwa penalti iliyokwamishwa nyavuni na Elias Pelembe baada ya Kevin Yondan kucheza rafu kwenye eneo la hatari. Mcha aliisawazishia Stars bao hilo dakika ya 65 akimalizia kazi nzuri ya Thomas Ulimwengu.
Mcha tena akaifungia Stars bao lililoelekea kuwa la ushindi dakika ya 71 kwa penalti, baada ya mabeki wa Mambas kumchezea rafu Mbwana Samatta kwenye eneo la hatari.
Stars iliongeza mashambulizi langoni mwa Msumbiji na kukosa mabao kadhaa ya wazi. Msumbiji walizinduka na kufanya shambulizi zuri lililowapatia bao la kusawazisha dakika ya 87 kupitia kwa Isaac Carvalho aliyetokea benchi pia.
Kwa matokeo, hayo Stars sasa itajitaji ushindi wa ugenini ili kusonga mbele, au sare ya kuanzia mabao 3-3, wakati wenyeji wanaweza kunufaika na sare ya 1-1 au 0-0. Ikiwa 2-2 tena, mshindi ataamuliwa kwa mikwaju ya penalti.
Kikosi cha Tanzania; Deogratius Munishi ‘Dida’, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mwinyi Kazimoto, Thomas Ulimwengu, Erasto Nyoni, John Bocco/Haroun Chanongo dk78, Mbwana Samatta/Simon Msuva dk83 na Mrisho Ngassa/Khamis Mcha dk57.
Msumbiji; Dario Khan, Momed Hagi, Zainadine Junior, Saddan Guambe, Francisco Mioche, Eduardo Jumisse/Isaac de Carvalho dk85, Elias Pelembe, Josemar Machaisse, Helder Pelembe, Almiro Lobo na Richard Campos.
Kwenye Marudiano huko Maputo, Msumbiji, Tanzania wanahitaji ushindi au Sare ya Bao 3-3 na kuendelea.
Kwenye Mechi nyingine iliyochezwa Leo huko Setsoto Stadium, Maseru, Wenyeji Lesotho waliifunga Kenya Bao 1-0 kwa Bao la Dakika ya 70 la Moletsane.
Mechi za Marudiano zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.
AFCON 2015-MOROCCO
RATIBA/MATOKEO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Julai 19
Uganda 2 Equatorial Guinea 0
Botswana 2 Guinea-Bissau 0
Sierra Leone 2 Seychelles 0
Jumapili Julai 20
Lesotho 1 Kenya 0
Tanzania 2 Mozambique 2
17:30 Congo v Rwanda
18:00 Benin v Malawi
** Mechi za Marudiano zitachezwa Wikiendi ya Agosti 1 hadi 3.
MAKUNDI:
KUNDI A
-Nigeria
-South Africa
-Sudan
-Mshindi Congo/Rwanda
KUNDI B
-Mali
-Algeria
-Ethiopia
Mshindi Benin/Malawi
KUNDI C
-Burkina Faso
-Angola
-Gabon
-Mshindi Lesotho/Kenya
KUNDI D
-Ivory Coast
-Cameroun
-Congo DR
-Mshindi Sierra Leone/Seychelles
KUNDI E
-Ghana
-Togo
-Guinea
Mshindi Uganda/Mauritania
KUNDI F
-Zambia
-Cape Verde
-Niger
-Mshindi Tanzania/Msumbiji
KUNDI G
-Tunisia
-Egypt
-Senegal
-Mshindi Botswana/Guinea-Bissau

Chapisha Maoni