Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Mwakirishi wa vilabu mkoani iringa TFF Kosta Magoroso amewataka wadau wa soka na wapenzi wa kandanda mkoani Iringa kwa ujumla kuakikisha wanachangia timu zao kwa maandishi ili kuepuka marumbano yasiyokuwa ya lazima pale inapotokea timu zimefanya vibaya kwa tatizo la pesa na wao wamechangia.

Magoroso alisema kwa takribani miaka 6 ambayo ni mwakilishi wa mkoa wa iringa TFF wadau wa soka mkoani Iringa wamekuwa wavivu kuchangia timu zao na jukumu zima la kuendesha timu hizo wanaachiwa viongozi ambao wanatwishwa mzigo moja kwa moja pindi timu ziofanyapo vibaya katika mchuano mbali mbali.

“nafahamu mpira wa Iringa toka nilipokuwa nikichea Lipuli mpira watu wa Iringa lazima Tubadilike tupepe mpira wetu,hakuna mtu wan je ambaye atakuja kusaidia sisi nawaomba sana,timu sio za viongozi ni timu za mkoa wa Iringa tukiwa makini tutafanya vizuri na sasa ivi tuna timu mbili za ligi daraja la kwanza kwa hiyo tuna nafasi kubwa ya kupandisha timu tujipange,kama unachangia changia kwa maandishi bila kusahau risti ili mwisho wa ijulikane pesa zimekwenda wapi.

Ni takribani miaka 14 imepita Toka Lipuli iliposhuka daraja  na harakati za timu hiyo kupanda daraja zimekuwa zikigonga mwamba mara kwa mara kutokana na maandalizi ya timu hiyo kuwa finyu tatizo kubwa likiwa ni pesaambapo kuna kipindi timu hiyo ilitaka kupotea kabisa kwenye ramani ya soka.


Chapisha Maoni