Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.










Timu ya soka ya lipuli ya Iringa inayoshiriki ligi daraja la kwanza imetangaza nafasi ya kocha ili kuziba pengo ambalo liliachwa na shadrack msajigwa  aliyeondoka baada ya kukinoa kikosi hicho kwa muda mfupi msimu uliopita.

Lipuli baada ya kuondoka msajigwa ilibakia mikononi mwa kocha msaidizi  ambaye aliifundisha timu hiyo ambayo ilifanya vizuri mzunguko wa pili na shadirack msajigwa alitimuka mara baada ya kutofautiana na viongozi wa timu hiyo.

Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI katibu msaidizi wa timu ya soka ya Lipuli Ronjino Malambo alizitaja moja ya sifa ambazo kocha wanaeimwitaji anatakiwa kuwa nazo ni pamoja kufundisha mpira zaidi ya mwaka mmoja ligi daraja la kwanza na kuendelea pia awe na cheti cha ukocha  daraja la kwanza.

“ufanisi katika kazi lazima anayeajiliwa lazima uwe mzuri  na iinatakiwa awe na uzoefu na kazi,sisi  tunataka kocha mwenye uzoefu sio  wa kujifuza  na lengo kubwa  ni kuifikisha lipuli mbali ya hapo ilipo, kwa soka la kisasa timu bila kuwa na mwalimu mzuri ni sawa na hakuna.

Kwa upande mwingine timu ya lipuli inatarajia kufanya uchaguzi wa viongozi wa timu hiyo tarehe 28 mwenzi wa tisa uchaguzi ambao ulitakiwa ufanyike mwenzi huulakini umehailishwa kutokana na maandalizi na tayari fomu za uchauzi zimeshaanza kutolewa    kwa nafsi 7 na sifa za wagombea ni pamoja na mgombea inatakiwa awe na umri wa miaka 25 na kuendelea,elimu ya kidato cha nne na kuendelea pia asiwe na tuhuma za makosa ya jinai katika kipindi chote cha maisha yake.

Awali uongozi wa lipuli ulilalamikiwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na timu kushindwa kufanya vizuri ambapo kwa sasa watu wanatakiwa kuchukua fomu kilingana na sifa zilizotajwa ili kuhakikisha wanapata nafsi ya kuongoza timu hiyo.



Chapisha Maoni