Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




TIMU ya Mkali Kids toka ziwani nyasa imefuzu kushiriki ligi daraja la tatu mkoa baada ya kufanya vizuri katika ligi daraja la nne wilayani nyasa ambapo timu hiyo ilifikisha alama 6 baada ya kushinda mechi mbili ambapo ligi hiyo ilikuwa ikishirikisha timu tatu tu.
Mchezo wa kwanza mkali kids waliifumua Young boys bao 2-1,kisha wakaifunga Bay Shooting Bao 3-0 kabla ya wao kufungwa bao 2-1 katika mchezo wa mwisho uliofanyika hivi karibuni ziwani humo ambapo wameungana na Bay shooting ambapo wataunga na mkali Stars pamoja na nyasa FC kuwalisha wilaya hiyo katika ligi daraja la tatu mkoa.
Akizungumza na jelamba viwanjani Kocha wa mkali kids muddy Songambele alisema kuwa hivi karibuni  wana ziara ya kwenda kucheza mpira maeneo ya chimate pamoja na nangombo ili kucheza mechi za kirafiki   ikiwa ni katika maandalizi ya kujiandaa na ligi Daraja la tatu mkoa kwa kuwa ligi hiyo inakuwa na upinzani mkubwa na yanaitajika maandalizi makubwa.
Timu za ziwani nyasa licha ya kuwa na vipaji vya kweli vya soka mara nyingi zinaishia ligi daraja la tatu mkoa kutokana na tatizo la maandalizi pamoja na hali ya miundombinu ya ziwani humo ingawa wana hamu kubwa ya kushiriki katika mashindano makubwa.


Chapisha Maoni