Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


BONDIA toka mkoani ruvuma Musa Omari maarufu kwa jina la chitepete amemchakaza bondia toka nchini Malawi Jonson Adamu Roundi ya pili katika pambano lisilokuwa la ubingwa la roundi 10 ambalo lilifanyika  katika uwanja wa maji maji Mjini songea.

Mchezo huo ambao ulishuudiwa na mashabiki wengi wa soka mjini humo, Omari alimaliza pambano hilo la kimataifa mapema baada ya kumpiga mmalawi Jonson Adam  ngumi ya chembe [upande wa moyo na akashindwa kuendelea na pambano na Omari akatangazwa mushindi.

Baada ya pambano hilo kumalizika musa Omari alisema mchezo wa ngumi ni mchezo anaupenda sana toka moyoni na endapo atapata udhamini wa kueleweka na kutafutiwa mapambano mengi na wachezaji wakubwa atakuwa tishio hapa nchini.

“kuwa nje ya Dar watu wanaweza kufikiria kuwa mimi sina uwezo wa kupigana lakini kiukweli mimi ninauwezo mkubwa na wale wote ambao wamenishuudia kwa macho yao wamejionea mwenyewe,nawaomba sana watanzania waniunge mkono siwezi kuwaangusha nipo pamoja nao.

Recodi ya Jonson Adam ndio imealibiwa kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na Musa Omari ambapo kabla ya hapo recodi yake mbaya ilikuwa ni kutoa sare mara mbili ambapo hakuwai kupoteza pambano lolote.


Chapisha Maoni