Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Candid, outspoken and supremely honest, and including interviews with those close to him, #2Sides is Rio's unique story: from his early days in Peckham, through to picking up the Champions League trophy on a rainy summer's night in Moscow, #2Sides is the tell-all account of an extraordinary and controversial life in the game. On winning and losing; on defending and attacking; on Moyes, management and fellow players; on John Terry, lost friendships and ongoing rivalries; on the love and hate of the beautiful game; and on playing for club, country and for yourself - this is a full spectrum of life at the very top of the footballing tree, and a superb retrospective of a truly fascinating career.
 
Baada kumshambulia Nahodha wa Chelsea John Terry na kumwita ‘Mpumbavu mkubwa’ kwa kumkashifu Kibaguzi Ndugu yake Rio, Anton Ferdinand, na kisha kukataa kuomba radhi, na pia kumlenga David Moyes, Meneja aliefukuzwa kazi Manchester United Msimu uliopita baada ya kudumu Miezi 10 tu, na kumweleza Moyes kama ‘mgeni’, ‘asiejua kazi’ na Mtu ‘hasi’, sasa Ferdinand amemgusia Sir Alex Ferguson.

Beki huyo wa zamani wa Man United mwenye Miaka 35 amesema Meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson alikuwa Gwiji wa Saikolojia ambae huwahamasisha Wachezaji wafanye vizuri.
Lakini upo wakati Ferguson na Rio walikwaruzana hasa kuhusiana na ile Skandali ya John Terry ambapo Kundi la Kupinga Ubaguzi Michezini, Kick It Out, walitayarisha Kampeni kwenye Mechi za Wikiendi moja ili Wachezaji wote wa Ligi Kuu England wavae Tisheti zilizoandikwa "One Game, One Community", yaani ‘Gemu moja, Jamii moja’’ kabla ya Mechi kuanza.

Kwenye Kitabu chake, Ferdinand anaeleza: “Kulikuwa hamna uwezekano mimi kuvaa Tisheti ile. Kundi lile lilikataa kwenda Kortini na sisi kumpinga Terry. Nisingeweza kuwaunga mkono kwa kuvaa Tisheti. Wazazi wangu pengine wasingeongea na mimi.”

Lakini Sir Alex Ferguson alimpinga Rio na kupandisha hasira huku akitumia maneno makali dhidi ya Ferdinand na kumpiga Faini ya Mshahara wa Wiki moja kwa kukataa kuvaa Tisheti.
Hata hivyo, Ferdinand alitoboa kuwa baadae alikutana na Ferguson na alistushwa pale Meneja huyo mwenye msimamo mkali alipoungama kuwa ni makosa kwake kumlazimisha Ferdinand kufanya kitu ambacho kiko kinyume na imani yake.

Ferdinand ameandika: “Nilivutiwa sana na jinsi alivyokubali kosa. Heshima yangu kwake ikazidi zaidi. Nadhani na yeye aliniheshimu zaidi kwa kusimama kidete kutetea kitu ninachoamini licha ya kuwepo presha kubwa.”

Baada kumponda sana mrithi wa Ferguson, David Moyes, Rio Ferdinand amemsifia sana Ferguson na kumweleza kuwa ni Mtu mwenye akili sana.

Ferdinand ameeleza Ferguson hakuogopa Wachezaji Mastaa kama Cristiano Ronaldo au Ryan Giggs tofauti na Mameneja wa England ambao walishindwa kunyanyua kidole dhidi ya Mastaa David Beckham, Steven Gerrard na Wayne Rooney.

Ferdinand anaeleza: “Yeye alikuwa Gwiji wa Saikolojia aliejua namna ya kumfanya kila Mchezaji acheze kiwango cha juu kabisa na kuwafanya wawe na akili ya ushindi tu. Aliwapa Watu imani kubwa ya kujaribu vitu na hakujali ukishindwa ili mradi uwe unajaribu kadri ya uwezo wako!”


Rio Ferdinand
Rio Ferdinand.jpg
Ferdinand playing for Manchester United in 2008.
Personal information
Full name Rio Gavin Ferdinand[1]
Date of birth 7 November 1978 (age 35)
Place of birth Denmark Hill, London, England
Height 1.89 m (6 ft 2 in)[2]
Playing position Centre-back
Club information
Current team
Queens Park Rangers
Number 5
Youth career
1992–1996 West Ham United
Senior career*
Years Team Apps (Gls)
1996–2000 West Ham United 127 (2)
1996–1997 Bournemouth (loan) 10 (0)
2000–2002 Leeds United 54 (2)
2002–2014 Manchester United 312 (7)
2014– Queens Park Rangers 4 (0)
National team
1996–1997 England U18 7 (0)
1997–2000 England U21 5 (0)
1997–2011 England 81 (3)


Chapisha Maoni