Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




Mmiriki wa ndanda Fc,maji ya Ndanda pia mjumbe wa NEC taifa CCM toka mkoani Iringa Mahamudu mwemsi  Madenge amemwaga vifaa vya michezo kwa Baadhi ya Timu Iringa Mjini ili kuendeleza kandanda mkoani Iringa.
Baadhi ya timu ambazo zimenufaika na vifaa hivyo ni pamoja na Mshindo Fc,Mlandege Fc  pamoja na Lipuli ambayo inajiandaa na ligi daraja la kwanza ambayo itaanza kutimua vumbi mwenzi wa kumi kwa nchi zima.
 
Akizungumza na Timu ya lipuli Fc  Madenge aliwataka viongozi wa lipuli kushirikiana bega kwa bega na wachezaji wa zamani waliopo hapa akiwemo Isihaka Majaliwa ambaye alicheza kwa mafanikio makubwa na Maji Maji ya Songea miaka ya 1980 bila kuwasahau wadau wa soka ili kuhakikisha timu hiyo inafanya vizuri katika michuano ya ligi daraja la kwanza msimu huu.
Pia aliwataka wachezaji wa timu hiyo kucheza mpira kwa kujituma ili kuinua vipaji vyao na kuepukana na mambo ya hanasa kama kunywa pombe pamoja na wanawake ili kutunza vipaji vyao na kufikia Marengo yao waliyojiwekea

“wachezaji lazima mcheze kwa bidii ili kukuza vipaji vyenu bila kujali hali ya kambi ya timu ipoje,pia vitu vingine kama pombe kwa wachezaji sio muhimu lazima mzingatie hilo,muda mwengine wachezaji hawataikiwi kuwa na simu kambini ili kujenga saikolojia ya wachezaji,na kuipuka kupokea taarifa zisizokuwa za lazima toka kwa watu wengine.

Madenge pia amewahaidi lipuli kuwaletea viatu bora toka ulaya kwaajili ya timu hiyo pamoja na vifaa vingine vya kufanyia mazoezi.


Chapisha Maoni