Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




KIUNGO wa Azam FC, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars akiitwa kwa mara ya kwanza chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij.
Nooij ametaja kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Morocco utakaochezwa Septemba 5, mwaka huu nchini Morocco.
 
Wachezaji wengine wapya katika kikosi hicho kutoka kile kilichotolewa na Msumbiji katika mechi ya mchujo ya Kombe la Mataifa ya Afrika ni kiungo Said Ndemla wa Simba SC na washambuliaji Mwagane Yeya wa Mbeya City na Juma Luizio wa ZESCO United ya Zambia.
 
Kikosi kamili ni makipa; Deogratias Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub (Yanga), Kelvin Yondani (Azam), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).
 
Viungo; Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).
 
Washambuliaji; John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio 9ZESCO, Zambia).
 
Kikosi hicho kinatarajiwa kuingia kambini Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) mchana katika hoteli ya Accomondia mjini Dar es Salaam na kitakuwa kikifanya mazoezi Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.


Chapisha Maoni