| ||||
Na Alex
Mapunda,Iringa
SHIRIKISHO
la soka hapa nchini TFF limesimamisha uchaguzi wa Lipuli ambao ulipangwa
kufanyika Tarehe 28 Septemba[jana] baada ya kubaini kuwa katiba ya Lipuli ina
mapungufu.
Akizungumza
na JELAMBA VIWANJANI
mwenyekiti wa uchaguzi wa timu hiyo Jackson Ibrahim Chaula alisema
taarifa ya kuhairishwa kwa uchaguzi waliipata masaa machache kabla ya uchaguzi
huo ambapo kwa sasa wanaeshimu maamuzi ya TFF na wanasubiri marekesho ya katiba hiyo.
“ni kweli
kulikuwa na mapungufu ambayo yalikuwepo kwenye katiba ya timu ya Lipuli na
marekebisho yalipelekwa Tff lakini Tff walichelewa kutupa majibu,ambapo kwa sasa tulipanga kutumia
katiba ya zamani suala ambalo Tff wamekataa.
Kwa upande
wake kaimu mwenyekiti pia mgombea wa
nafsi ya mwenyekiti bwana Renatus Kalinga ilisema kuwa hizo ni nyama za watu wachache
ambao wapo karibu na Tff wasioitakia mema timu ya Lipuli na wanatarajia kukaa
kikao ili kujua hatima ya timu ya Lipuli kwa kipindi hiki ambacho inaitaji
msaada mkubwa ikiwemo wao kujiuzulu na
kuwaachia wanachama wafanye maamuzi yao.
Awali uchaguzi huo ulitakiwa
kufanyika tarehe 28 mwenzi wa nane lakini wasimanizi waliamua kuahirisha
kwa kuwa maandalizi hayakukamirika lakini mwenzi huu imeshindikana tena suala
ambalo linaweza likaigharimu timu hiyo kwa kuwa inaitaji usimamizi wa karibu
sana, kuelekea kwenye kinyang’anyiro cha ligi daraja la kwanza mwenzi wa kumi.
Chapisha Maoni