Mechi za klabu bingwa barani Ulaya
iliendelea usiku wa kuamkia Alhamis wakati timu kadhaa ziliposhuka dimbani.
Vijana wa mzee Wenger, Arsenal,
ulikuwa usiku wao baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Galatasaray
ya Uturuki, huku mchezaji mpya wa timu hiyo Danny 'Electric' Welbeck akiondoka
na mpira baada ya kuzifumania nyavu za wapinzani wao mara tatu, moja likifungwa
na Allexis Sanchez.
Katika mchezo huo Arsenal walimaliza
pungufu baada ya kipa wao Wojciech Szczeny kutolewa kwa kadi nyekundu katika
dakika ya 60 ya mchezo.
Wakati hayo yakijiri vijogoo wa
Anfield Liverpool walikuwa ugenini huko Uswis na kujikuta wakiangukia pua baada
ya kufungwa bao 1-0 na FC Basel.
Mabingwa watetezi Real Madrid
waliendeleza wimbi la ushindi kwa kuisasambua Ludogorets Razgrad ya Bulgaria
kwa jumla ya mabao 2-1. Christiano Ronaldo na Kareem Benzema ndio waliopeleka
ushindi kwa vijana hao wa Benabeu.
Kwingineko Atletico Madrid
waliialika Juventus ya Italia, hadi mwisho wa mchezo Atletico ikaibuka na
ushindi wa goli 1-0.
Borusia Dotmund wakaikaanga
Anderlecht kwa mabao 3-0. Bayern Liverkusen wakaiangamiza Benfica kwa mabao
3-1, huku Malmo FF ya Sweden wakawaduwaza Olympiakos ya Ugiriki kwa mabao 2-0.
Champions League - Group B October 1
|
|||
FT
|
Basel
|
Liverpool
|
|
FT
|
PFC Ludogorets Razgrad
|
Real Madrid
|
Champions League - Group C October 1
|
|||
FT
|
Zenit St. Petersburg
|
Monaco
|
|
FT
|
Bayer Leverkusen
|
Benfica
|
Champions League - Group D October 1
|
|||
FT
|
Anderlecht
|
Borussia Dortmund
|
|
FT
|
Arsenal
|
Galatasaray
|
Chapisha Maoni