Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Mjumbe wa zamani wa shirikisho la soka duniani amesema kuwa heshima ya Fifa haitaweza kurudi mpaka pale Rais Wa shirikisho hilo Sepp Blatter atakapoachia ngazi.
Michael Hershman ameiambia BBC kuwa Sepp blatter hanabudi kuondoka na kupisha mtu mwingine kukiongoza chombo hicho.
Amedai kuwa hivi sasa yanatakiwa mabadiliko ya uongozi baada ya Fifa kuwa katika mlolongo wa shutuma za rushwa kwa miaka mingi,hivyo basi ni vyema uongozi ukabadilika.
Blatter amekuwa Rais wa shirikisho hilo tangu mwaka 1998 na mwezi uliopita alitangaza nia ya kuwania tena nafasi hiyo ingawa aliahidi kuwa awamu ya nne ambayo ni sasa, ni ya mwisho.
Hershman amesema anasikitishwa mno na hatua ya wadau wa nje hasa wadhamini kutoingilia kati na kuchukua hatua stahiki, badala yake wamekuwa wakitoa taarifa kwa vyombo vya habari wakisema wanatarajia kuona FIFA ikitekeleza majukumu yake kwa kufuata maadili.
by bbc


Chapisha Maoni