Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Ligi kuu ya vodacom Tanzania bara inatarajia kuwaka moto leo katika viwanja tofauti ambapo bingwa matetezi na kinara wa Ligi , Azam FC, leo wako kwao Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam kuivaa JKT Ruvu ambayo ipo Nafasi ya 11 katika msimamo wa ligi hiyo.


 Baada ya kutoka 0-0 katika Dabi yao, Yanga na Simba Wikiendi hii zote ziko ugenini kwa Yanga kucheza huko Kambarage, Shinyanga na Timu iliyopanda Daraja Msimu huu Stand United wakati Simba wako huko Sokoine, Mbeya kuivaa Prisons wapizani wao wa miaka mingi.

Mechi nyingine za Jumamosi zitachezwa huko Nangwanda, Mtwara kati ya Wenyeji Ndanda FC dhidi ya Mgambo JKT na kule Kaitaba, Bukoba kati ya Kagera Sugar na Coastal Union wakati huko Mabatini, Mlandizi Ruvu Shooting itakipiga na Polisi Moro.
Jumapili itakuwepo Mechi moja tu na kali sana huko Sokoine, Mbeya wakati Mbeya City itakapoumana na Mtibwa Sugar.
RATIBA LIGI KUU YA VODACOM


25.10.2014
29
STAND UNITED
Vs
YOUNG AFRICANS
25.10.2014
30
NDANDA FC
Vs
MGAMBO JKT
25.10.2014
31
KAGERA SUGAR
Vs
COASTAL UNION
25.10.2014
32
AZAM FC
Vs
JKT RUVU
25.10.2014
33
TANZANIA PRISONS
Vs
SIMBA SC
25.10.2014
34
RUVU SHOOTINGS
Vs
POLISI MOROGORO
26.10.2014
35
MBEYA CITY
Vs
MTIBWA SUGAR


MSIMAMO
1
Azam431061510

1
Mtibwa Sugar431061510

3
Coastal Union42116427

4
Young Africans42114407

5
Kagera Sugar41213215

6
Mbeya City41211105

7
Stand United412135-25

8
Simba SC40404404

8
Tanzania Prisons41124404

10
JKT Ruvu411235-24

10
Ruvu Shooting411235-24

12
Ndanda410379-23

13
Polisi Morogoro403135-23

14
Mgambo JKT410314-33


Chapisha Maoni