lipuli kicheko,kurugenzi kilio.
Na Alex Mapunda,Iringa
BAADA ya kufunya vibaya katika mechi zao za hawali timu ya Lipuli
toka Iringa imezinduka usingizini na kuichakaza African Lyon kwa kichapo cha
bao 1-0 katika mchezo wa ligi daraja la kwanza uliofanyika kwenye uwanja wa
karume Jijini Dar es salam.
Katika mchezo huo ambao Lipuli walicheza kwa tahadhari kubwa
kubwa ili kuepuka kufanya vibaya kwa mara nyingine bao pekee la Lipuli ambapo lilipeleka
kilio kwa wapizani wao lilifungwa na Abdala
shauli na likadumu hadi dakika ya mwisho ya mchezo.
Hadi kufikia hivi sasa Lipuli imeshuka dimbani mara tatu
ambapo mchezo wa kwanza walifungwa bao 2-1 dhidi ya Friends Rangers kabla ya
kutoka sare na African Sports toka Tanga.
Kwa upande wa Kurugenzi wa mafinga wao wamejikuta wakikung’utwa
bao 2-1 katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya wauza mitumba Ashanti United
katika uwanja wao wa nyumbani na kuanza kupoteza matumaini ya kufanya vizuri
kwa kuwa takwimu yao inaonyesha inashuka ambapo mchezo wa kwanza walishinda bao
2-0 dhidi ya Tessema Fc,mchezo wa pili wakatoka sare na mchezo wa mwisho
wamechezea kichapo.
Kindumbwe ndumbwe cha ligi daraja la
kwanza kimeanza kutimua vumbi mapema mwenzi huu wa kumi ambapo safari hii
kuna makundi mawili na Kundi A lina timu za African Lyon, African Sports,
Ashanti United, Friends Rangers, Kimondo SC, Kurugenzi Mafinga, Lipuli,
Majimaji, Mlale JKT, Polisi Dar es Salaam, Tessema FC na Villa Squad.
Wakati kundi B lina timu za Burkina Faso, Geita Veterans SC, Green Warriors, Kanembwa JKT, Mwadui SC, Oljoro JKT, Panone FC, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora, Rhino Rangers na Toto Africans. Ratiba ya Ligi hiyo itatolewa hivi
Chapisha Maoni