Na A lex Mapunda,Iringa
TIMU ya soka ya Lipuli imeamishia kambi yake Jijini
Dar esalam ili kujianda vyema na michuano ya ligi Daraja la kwanza
inayotarajiwa kutimua vumbi mapema mwenzi huu.
Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI Katibu Msaidizi wa
timu hiyo Ronjino Malambo alisema Timu ya Lipuli Ikiwa Dar es salam itacheza
mechi za kirafiki ili kuimalisha zaidi kikosi cha timu hiyo ambapo wakati wa
ligi Dar es salam watacheza mechi mbili na nyingine wataenda kucheza na African
Sports mkoani Tanga kabla ya kurudi nyumbani Iringa ili kuendelea na michezo
mingine.
“wadau tunawaomba sana wasitarajie miugiza timu aiwezi kufanya vizuri bila wao kutoa
michango ,sisi hatutaki pesa pekee hata mwenye mchele,ndizi,unga tunaomba
atuletee ili timu iweze kufanya vizuri na kuutangaza vyema mkoa wa Iringa,kuhusu
kambi ya jijini Dar kila kitu kimeenda vizuri hadi uwanja wa mazoezi tumepata”alisema
malambo.
Kindumbwe ndumbwe cha ligi daraja la
kwanza kinatarajia kutimua vumbi mapema mwenzi huu wa kumi ambapo safari hii
kutakuwepo na makundi mawili na Kundi A lina timu za African Lyon, African
Sports, Ashanti United, Friends Rangers, Kimondo SC, Kurugenzi Mafinga, Lipuli,
Majimaji, Mlale JKT, Polisi Dar es Salaam, Tessema FC na Villa Squad.
Wakati kundi B lina timu za Burkina Faso, Geita Veterans SC, Green Warriors, Kanembwa JKT, Mwadui SC, Oljoro JKT, Panone FC, Polisi Dodoma, Polisi Mara, Polisi Tabora, Rhino Rangers na Toto Africans. Ratiba ya Ligi hiyo itatolewa hivi punde.
Chapisha Maoni