Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Na Sophia Mwaipyana,Mbeya
 
  Mchezaji wa Mbeya City Sadi Kipanga ambaye alikuwa majeruhi   kulejea  kuwavaa Azam Fc kesho baada ya kupona majelaha.
 
Akiongea na Championi msemaji wa timu hiyo Disimas Ten alisema kuwa  Sadi Kipanga na Alex Seti  ambao walikuwa majeruhi na hawajacheza toka ligi iyanze wameshapona  nawanatalajia  kucheza mchezo dhidi yao na Azam.
 
“Kulejea kwa  wachezaji hao  kunatupa matumaini makubwa ya kutoka naushindi  kwani kuna nguvu itaongezeka katika kikosi hicho kwani nikati ya wachezaji wenye uwezo mzuri.”
 
Akizungumzia upande wa maandalizi ya kikosi hicho Ten alisema kuwa   mwalimu alikuwa akifanya marekebisho katika safu ya ushambuliaji  katika hii wiki moja tuliyokuwa hakuna mechi.
 
“Natumepata  mechi ya majaribio   ambayo tulicheza na timu ya Combine ya Kyela na tulitoka na ushindi wagoli saba  kwahali hiyo  tunapata picha nzuri ya mchezo wakesho  pale tulipokuwa na mapungufu tumesha fanya marekebisho.”
 
 
“Mechi yakesho ni mechi ngumu lakini  siyo kwamba Azam nibora  kuliko sisi  mwakajana walitufunga kiutatauta tuu  lakini kwamechi ya kesho wasitegeme kutoka na ushindi tukiwa nyumbani .”
 
Kwaupande wa mashabiki wa tawi la Sido Fc waliwataka mashabiki waje kwa wingi kuona staili yao mpya ya ushangiliaji  .
 
Mwisho


Chapisha Maoni