MAHAKA ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salam imeruhusu michuano ya miss Tanzania 2014 ambayo ilipangwa kufanyika kesho kutwa ifanyeke kama ambavyo ilipangwa.
Hakimu mkazi frank moshi ametoa maamzi hayo baada ya kusikiliza kwa makini ombi ambalo liliwasiliswa na mwazilishi wa mashindano hayo prashant patel,na kusema kuwa kusimamisha mashindano hayo kutawagharimu watu wasio na hatia wakiwemo wadhamini,hivyo hakuna umuhimu wa kusimamisha.
MSHINDI wa shindano la Redd’s Miss
Tanzania 2014 ataondoka na kitita cha sh. Mil.18 imefahamika.
Hayo yaMEsemwa leo na Meneja
wa Kinywaji cha Redd’s Premium Cold ambao ndiyo wadhamini wakuu wa
shindano hilo Victoria Kimaro katika mkutano na waandishi wa habari
uliofanyika kwenye ukumbi wa JB Belmont
Jijini Jijini Dar es Salaam.
Kimaro alisema kwamba huu ni mwaka
wao wa mwisho wa udhamini katika shindano hilo hivyo wameamua kumpa
mshindi fedha taslimu Mil.8 pia Mil. 10 ambayo ilikua anunuliwe gari nayo
atapata fedha taslimu ili kama ataamua kununua gari ama kuweza kujilipia ada ya
shule ama kufanya biashara hiyo itategea maamuzi ya mshindi huyo.
Kimaro anazitaja zawadi za warembo
wengine kuwa ni atakayeibuka kuwa mshindi wa pili atapata kitita cha
Mil.6, mshindi wa tatu atapata Mil.4.2
mshindi wan ne atapata Mil 3.2 wakati
mshindi wa tano atapata Mil.2.2.
Warembo watakaoshika nafasi
ya 6 hadi 15 wote kila mmoja taondoka na
kitita cha Mil.1.2 huku wengine kuanzia wa 16 hadi 30 watapata kifuta jasho cha
sh.700,000 kila mmoja alisema Kimaro.
Aidha aliongeza kwa kusema
kuwa katika shindano hili burudani kubwa
itatolewa na msanii Omary Nyembo ‘Ommy
Dimpoz’ na wapambe wake na mwanamuziki anayetamba hivi sasa Vanessa Mdee .
Kimaro amesema kwamba maandalizi
ya shindano hilo yamekamilika huku ukumbi wa Mlimani City ukiwa katika hatua
nzuri za maandalizi ikiwemo kutengeneza jukwaa la aina yake.
Aliongeza kwa kusema kuwa licha ya
kuwa wao wanamaliza mkataba na Lino lakini mrembo atakayeshinda atapata stahili
zote aikiwemo kupata posho za kazi mbalimbali za akijamii ambazo atakuwa
akizifanya kabla ya kwenda kuiwakilisha nchi kwenye shindano la kumsaka mrembo
wa dunia (Miss World).
Wakati huohuo Mkurugenzi wa
Kampuni ya Lino International Agency Limited ambao ndiyo waratibu wa
shindano hilo Hashim Lundenga alisema kwamba tiketi zimeanza kuuzwa katika
maduka ya vipodozi ya Shear Illusions, Mlimani City na Millenium Tower
Makumbusho Jijini Dar es Salaam.
Jumla ya warembo 30 wanawania taji
hilo ambalo linashikiliwa na Redd’s Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa.
Chapisha Maoni