Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




HILO NI SOKA LA TANZANIA
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imemfungia wakili Damas Ndumbaro kujihusisha na mambo ya soka kwa muda wa miaka saba na faini ya kiasi cha fedha.

Ndumbaro ambaye aliingia katika mzozo mkubwa na Rais wa TFF, Jamal Malinzi wiki iliyopita baada ya TFF kuagiza kila klabu kukatwa asilimia tano za mapato yatokanayo na udhamini wa klabu hizo wanaoupata kutoka kwa Vodacom, wadhamini wakuu wa ligi kuu ya Tanzania Bara, na Azam TV.

Ndumbaro alikimbilia katika vyombo vya habari na kusema wazi kuwa, klabu zimemuagiza kuwaambia TFF kuwa havipo tayari na havitakubali jambo hilo litokee, huku akijiamini na kuchambua baadhi ya vipengele na mambo ya sheria, Ndumbaro alivuka mipaka pale aliposema kuwa wanatafuta wastani wa wajumbe wa mkutano mkuu wa TFF na kupiga kura ya kutokuwa na imani na rais wa shirikisho, Malinzi.

Kikao cha juzi cha kamati ya nidhamu kimefikia uamuzi wa kumfungia, Ndumbaro na kumlilipisha faini kwa sababu, Ndumbaro ambaye alizungumza kama wakili wa klabu za ligi kuu kupitia,.

TFF imedai Ndumbaro amekanwa na klabu ingawa taarifa zinaeleza si kweli kwa kuwa viongozi wa klabu 12 walisaini kumpitisha kuwa wakili wao.



Akieleza namna kesi hiyo ilivyoendeshwa kabla ya kutoa hukumu hiyo, Msemwa alisema wamesikiliza kesi hiyo kwa siku mbili; Jumamosi na Jumapili na hukumu ilitolewa bila uwapo wa mlalamikiwa.

Amesema baada ya kupelekewa malalamiko ya Sekretarieti ya TFF dhidi ya Ndumbaro, walimpelekea barua mlalamikiwa na kumtaka kufika kwenye kikao Oktoba 10. Amesema Ndumbaro hakufika mbele ya kamati hiyo lakini walipata taarifa za kutofika kwakew kutoka kwa wakili wake, Nestory Peter.
“Kwa kuwa Ndumbaro hakufika mbele ya kamati, tuliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 11 mwaka huu kujadili kama tunaweza kutoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja ama la. Kwa kuwa Ndumbaro hakuleta ushahidi wowote kueleza mahali alipo, kamati iliamua kusikiliza kesi ya upande mmoja na kutoa hukumu,” amesema.
Akielezea ushahidi wa TFF uliowasilishwa na Mvella mbele ya kamati, Msemwa TFF imedai kuwa Ndumbaro alikiuka Kanuni za Nidhamu na Kanuni za Ligi za TFF kwa kuzisemea klabu, serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kuituhumu TFF kuziiibia klabu, serikali na CCM kupitia makato ya milangoni huku akitishia kulishtaki shirikisho FIFA.
Aidha, Msemwa amesema TFF walidai Ndumbaro kama mwanachama wa shirikisho, amekiuka Kanuni za Ligi toleo la 2014 kwa kuwataka wadhamini wakuu wa ligi kuu, Kampuni ya Huduma za Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na Kampuni ya Azam Media waliyonunua matangazo ya televisheni ya ligi hiyo kujitoa.
Amesema kuwa Mvella aliwasilisha ushahidi wa sauti iliyorekodiwa na Clouds FM na magazeti na likiwamo gazeti la NIPASHE la Oktoba 4 , mwaka huu lililotumika kama ushahidi Na. 4, gazeti la Jambo Leo, Tanzania Daima, Daily News na The Citizens yakinukuu kauli za Ndumbaro dhidi ya TFF.
Msemwa pia amesema mlalamikaji aliwasilisha barua za klabu za Coastal Union ya Tanga na Stand United ya Shinyanga zilizotumwa TFF zikikana kumtuma Ndumbaro kutoa tamko hilo.
Hata hivyo, Makamu Mwenyekiti wa Coastal, Steve Mguto alikuwa miongoni mwa wawakilishi wa klabu kwenye Ukumbi wa Golden Jubilee jijini Dar es Salaam wakati Ndumbaro akitoa tamko hilo dhidi ya TFF.





Chapisha Maoni