Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.







Na Sophia Mwaipyana,Mbeya
 
Washambuliaji  wawili  waTanzania Prisons waliyokuwa majeruhi   Frank William na Peter Michael wameanza mazoezi mepesi  kwajili ya kuwavaa maafande wenzao kutoka mkoani Pwani Jkt Ruvu.
 
Meneja wa timu hiyo Enock Mwanguku alisema kuwa  ambao walikosa mchezo uliyo pita dhidi ya Azam Fc  sasa wapo tayari kwamchezowajumapili  utakao chezwa katika uwanja wa sokoinne jijini Mbeya.
 
“Wachezaji wetu wawili kati ya wale wanne ambao walikuwa majeruhi wameanza mazoezi  mepesi  tunategemea kufiki siku ya mchezo watakuwa  wako vizuri.”
 
 
Akiongelea kwa upande wamaandalizi dhidi ya mchezo huu alisemakuwa kikosi kiko tayari kuwakabili  Jkt Ruvu kutoka mkoani Pwani  kwani moalali ya wachezaji  ipo juu.
 
 
 
 
 
Tanzania prisons ambao wanashuka dimbani kwamara ya pili katika uwanja wao wanyumbani dhidi ya Jkt Ruvu mpaka hivi sasa wamejikusanyia pointi nne mara baada ya kushuka dimbani mara tatu.


Chapisha Maoni